Ticker

6/recent/ticker-posts

MRATIBU WA UN NCHINI, ALVARO RODRIGUEZ ZIARANI MKOANI SINGIDA KUKAGUA MIRADI YA SHIRIKA HILO

IMG_4020
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake jana mjini Singida.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo.
Mratibu huyo yupo Mkoani hapa kwa siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika siku yake ya kwanza atatembelea mradi wa afya ambao unashughulikia watu wanaoishi na VVU katika kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi. Pia atatembelea kikundi cha ufugaji nyuki kinachojihusisha na uzalishaji wa asali na utengenezaji wa mishumaa.
Aidha akiwa kijiji cha Puma atatembelea kambi waliokolazwa watu wenye ugonjwa wa Kipindupindu.
Katika ukaguzi wa miradi hiyo Mratibu huyo atapata nafasi ya kuzungumza na walengwa wa miradi hiyo ili kupata mafanikio na changamoto zilizojitokeza.
Katika siku yake ya pili na ya mwisho mkoani Singida Bw. Alvaro Rodriguez atatembelea mradi mkubwa wa ufugaji nyuki kisasa unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).
Baada ya hapo atatembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa inayoendelea kujengwa kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alitoa Shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa misaada yake ya kuisaidia serikali katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo ameomba Mashirika hayo yaendelea kusaidia katika Nyanja za upatikanaji wa ajira kwa vijana na masoko kwa wakulima.
Mratibu huyo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Singida ataelekea mkoa wa Tabora ambapo ataanza ziara yake tarehe 3 mwezi Desemba na baada ya kumaliza mkoa wa Tabora atelekea mkoani Kigoma tarehe 4 hadi 6 nwezi Desemba.
Singida ni kati ya mikoa itakayounufaika na mpango mpya wa malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa 2016-2030.
IMG_4026
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisalimiana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) aliyeambatana na Bw. Rodriguez. Aliyeketi ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe.
IMG_4039
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa kwanza kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes. wengine pichani ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa kwanza kulia).
IMG_4034
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisoma baadhi ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha 'Mwongozo wa wadau wa kilimo na mifugo' kilichoandaliwa na ofisini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani). Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe.
IMG_4042
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akitoa maelezo ya lengo namba 3 ambalo ni 'Afya Njema na Ustawi' wakati wa kutambulisha malengo mapya ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone walipomtembelea ofisini kwake jana.
IMG_4065
Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe akioorodhesha mambo muhimu yanayotakiwa kufanyika katika mkoa wa Singida ili kufanikisha utekelezaji wa lengo namba 3 ambalo ni 'Afya Njema na Ustawi' kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa 2016-2030. Wanaoshuhudia tukio hilo kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan.
IMG_4072
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa kwanza kulia), Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa pili kulia) pamoja na Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes (wa tatu kushoto) wakimkabidhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez bango hilo lenye mambo muhimu yanayotakiwa kufanyika katika mkoa wa Singida ili kufanikisha lengo namba 3 kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) aliyeambatana kwenye ziara hiyo na Afisa a Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (katikati kulia).
IMG_4080
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa pili kulia), Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) kwenye bango maalum lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yanayotakiwa kumfikia kila mwananchi nchini kwa ajili ya utekelezaji.
IMG_4086
Kutoka kushoto ni Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo Kang'ombe, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw. Sute pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan.
IMG_4096
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo wa mkoa.
IMG_4092
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone.
......AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI SINGIDA......
IMG_3987
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameambatana na Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kulia) mara baada ya kusimamisha gari maeneo ya Babati mjini.
IMG_3988
Neema Mikaeli (22)akihamaki kuona watu waliokuwa wakimsogelea (hawapo pichani) katika eneo alilokuwa akifua nguo kwenye dimbwi la maji machafu ya mvua kama yanavyoonekana pichani.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akiwa njiani kuelekea mkoani Singida alishtushwa kuona mkazi mmoja wa Babati mjini Neema Mikaeli (22) akifua nguo kwenye dimbwi la maji machafu ya mvua na kusimama na kuzungumza nae ambapo aligundua kuna tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na ukataji miti ambao unapelekea kuharibu mazingira.
Katika mazungumzo ya Neema alisema kuwa kuna mabomba ya maji yaliyowekwa zaidi ya miaka 3 sasa lakini hayatoi maji na hivyo kupelekea wao kutembelea umbali mrefu ambao kuna mto na wanatumia maji ya mto huo kupikia na kunywa.
Akiongea na Mikaela alimuhakikishia kwamba Umoja wa Mataifa utazidi kufanya kazi ka ukaribu na serikali ya Tanzania sambamba na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
IMG_3995
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Ofisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu wakizungumza na Mkazi huyo wa wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara, Neema Mikaeli (22) aliyekuwa akifua nguo zake kwenye dimbwi hilo kutokana na kukosekana kwa maji katika eneo lao.
IMG_4000
Haya ndio maji ambayo hata sabuni ya unga haikolei yaliyokutwa yakitumiwa na Neema Mikaeli (22) (hayupo pichani) kufulia nguo zake.
IMG_3983
Neema Mikaeli (22) akiwa kwenye eneo la dimbi la maji ya mvua akiendelea kufanya usafi wa nguo zake.

Post a Comment

0 Comments