Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imesherekea sherehe za Uhuru wa Tanganyika, Disemba 9 kwa kufanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach kama jinsi alivyoagiza rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuagiza kuwa siku ya Uhuru itumike kufanya usafi kutokana na kushamiri kwa uchafu katika mazingira yanayotuzunguka.
Kwa kufata agizo hilo la Dkt. Magufuli, MeTL Group kwa kujumuisha viongozi wa kampuni na wafanyakazi wake imefanya usafi kwa pamoja katika ufukwe wa Coco Beach ili kusafisha eneo hilo ambalo linatumiwa na watu wa aina mbalimbali kwenda kujipumzisha pamoja ndugu na familia siku za mapumziko.
Hizi ni baadhi ya picha wakati wafanyakazi wa MeTL Group wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach;
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer (kulia) akiongoza na Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Kijumbe kuelekea kwenye eneo la usafi mara baada ya kuwasili kwenye fukwe za Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote Dec 9, 2015.
Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL Group wakiwasili kwenye fukwe za Coco Beach kushiriki zoezi la usafi.
#HapaKaziTu........Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer (kulia) akisaidiana na Kiongozi Mahusiano ya Kazi wa MeTL Group, Subrina Gulamali Bhatti kubeba moja ya gogo lililokuwa linazagaa kwenye fukwe hizo.
Wafanyakazi wa makampuni ya MeTL Group wakiendelea na zoezi la usafi katika fukwe za Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote Dec 9, 2015.
Zoezi la kukusanya takataka na kuchoma mifuko ya nailoni iliyokuwa imezagaa kwenye fukwe za Coco Beach likiendelea.
Wengine wakiendelea kufyeka vichaka vya majani katika fukwe za Coco Beach.
Zoezi likiendelea.
Takataka zikiendelea kukusanywa na kuchomwa moto.
Takataka zikikusanywa kwenye viroba.
Zoezi likiendelea kwa ushirikiano wa hali ya juu.
#HapaKaziTu ndio maneno waliyokuwa wakisema wafanyakazi wa MeTL Group wakiendelea na zoezi la kusafisha fukwe za Coco Beach jijini Dar.
Baadhi ya wafanyakazi wa MeTL Group katika picha ya pamoja.
Picha za kumbukumbu baada ya kazi zilipigwa.
Mkuu kitengo cha Rasimali watu anayeshughulikia wafanyakazi wa ndani (Local) kampuni ya MeTL Group, Masuma Mushtak (waliosimama wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Makao Makuu ya Ofisi za MeTL Group.