Ticker

6/recent/ticker-posts

WATAKAIWA KUTOA DAWA ZINAZOHITAJIKA

Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji
ngozi waMji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,
wakiwa kwenye kongamanola uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa
wajasiriamali na vikundivilivyosajiliwa (Kikoa)
 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Mkoani Manyara,
Isaya Shekifu akizungumza jana katika kongamano la uhamasishaji wa mpango
wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo
Mahamoud Kambona na kushoto ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii
(CHF) mkoani humo Reginald Kileo

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambonaakizungumza
wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima yaafya wa
kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo
waMirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Nchini (NHIF) wa mkoahuo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya
Moipo Joseph Mtataiko

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa Mkoawa
Manyara, Isaya Shekifu akiandika maswali yaliyokuwa yanaulizwa katika
kongamano la uhamasishaji wampango wa bima ya afya wa kikoa kwa
wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mjimdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro. 
Na Woinde Shizza
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaasa
viongozi wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuishinikiza
bohari ya dawa nchini (MSD) kutoa dawa zinazohitajika.


Kambona aliyasema hayo jana mji mdogo wa Mirerani kwenye uzinduzi wa
kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na
vikundi vilivyosajiliwa (Kikoa).


Kambona alisema amepata malalamiko kwenye vituo vya afya Mirernai na
Orkesumet kuwa wamekuwa wanaomba dawa MSD na kuzilipia lakini wanapatiwa
dawa ambazo hawana mahitaji nayo hivyo kupata hasara.


“Haina maana watu waagize dawa za malaria wao wawape dawa za kuvimba miguu
zisozohitajika, ila NHIF mpo karibu na watu wa MSD, zungumzeni nao ili
watoe dawa zinazoombwa na siyo kwa matakwa yao,” alisema Kambona. 


Pia, alivitaka vikundi vya ushirika wa Saccos, Vicoba, Amcos, Vibindo,
wachimba madini, waendesha bodaboda, mama na baba lishe na wasindika ngozi,
wajiunge na bima ya afya ya Kikoa ili wapatiwe matibabu kwa unafuu. 


*Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani Manyara
Isaya Shekifu  alisema mpango huo wa kikoa utamwezesha mwanachama wa
kikundi kupata matibabu yote kama watumishi wa serikali wanavyopata kwenye
zaidi ya vituo 6,000 nchini nzima kwa mchango mtu mmoja sh76,800 kwa mwaka.
*


*Shekifu alisema gharama za matibabu nchini zinapanda kila uchao na huwa
vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzimudu pindi anapougua, bali
kupitia kikoa wajasiriamali nchini watanufaika kupitia matibabu
watakayoyapatiwa.*


*“Ugonjwa haupigi hodi bali humpata mtu wakati wowote na gharama za
matibabu zipo juu, ila kupitia kikoa wajasiriamali watapata matibabu bila
tatizo lolote, hivyo wanapaswa kujiunga kwa wingi kwenye bima hii,”
alisema.*


*Mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani Manyara, Reginald
Kileo alitaja mafao hayo yatahusisha* *gharama za kujiandikisha kumuona
daktari, dawa zote zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
vipimo vidogo na vikubwa kama MRI na CT Scan, kulazwa na miwani ya kusomea.*



*“Mafao mengine ni upasuaji mdogo na mkubwa na upasuaji wa kujifungua kwa
wanawake, matibabu ya kinywa na meno, matibabu ya macho, mazoezi ya
kimatibabu ya viungo (physiotherapy) na vifaa saidizi kama magongo na
vishikizi vya shingo,” alisema Kileo. *

Post a Comment

0 Comments