Mwanamuziki Fid Q akitoa burudani
katika moja ya tamasha la Coke Studio
-Wanafunzi na vijana mitaani
waendelea kupata burudani
Onyesho la Coke Studio msimu wa tatu linaloendelea
linazidi kuleta burudani na furaha kwenye makundi mbalimbali ya jamii na kuacha
gumzo kwa wengi nchini.
Vijana wengi wameeleza kuwa pamoja na kuburudika na maonyesho ya kolabo za wanamuziki machachari
yanayoonyeshwa kupitia luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi na kwenye redio
ya Clouds bado wamekuwa wakipata burudani kutoka matamasha shirikishi
yanayoendelea kwenye mikoa mbalimbali na kushirikisha watu kutoka makundi
mbalimbali ya jamii.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walipohojiwa juu ya
onyesho hili walisema kuwa linaleta raha na burudani huku likiibua vipaji na
kuwakutanisha vijana na watu wanaojiamini ambao wamefanikiwa kwenye mambo
wanayoyafanya.
“Coke Studio ni zaidi ya burudani kwa kuwa pia
inatuwezesha vijana kuonyesha vipaji wakati huo huo kukutana na watu ambao
wanajiamini ambao wamefanikiwa katika mambo yao”.Alisema Willy Chale Mwanafunzi
wa Sekondari ya Mwanza.
Miriam Chande mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa fedha
alisema analipenda onyesho la Coke Studio kwa kuwa linatoa burudani ya aina
yake ya muziki ambayo imewalenga vijana na inawawezesha kupata jumbe za
kuwahamasisha kusonga mbele kimaendeleo.
Kassim Juma,mwendesha bodaboda na mwanamuziki wa
kujitegemea amesema kuwa yeye na wenzake wanapenda onyesho la Coke Studio kwa
kuwa ni la viwango na limelenga kutoka burudani kwa makundi mbalimbali kupitia kuangalia kolabo
za wanamuziki na matamasha ya muziki na burudani yanayoendelea sehemu
mbalimbali nchini.
Msimu wa Coke Studio mwaka huu umeshirikisha wanamuziki
mbalimbali kutoka Tanzania na nchi za nje
Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up)
na Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na
mwanamuziki 2face kutoka Nigeria , Ali Kiba na
Victoria Kimani na Ben Paul na wangechi.
Msimu huu wa Coke Studio umeambatana na kampeni mpya yenye
jina la ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, na hivyo kujumuisha vijana mbalimbali
ambao wanaamini katika kufikia malengo yao bila ya kujali changamoto
zinazowakabili.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa
pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo
tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii
wachanga kushirikiana na wakubwa ili
kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji
vyao
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia