Meneja
Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki (kushoto ) na Mkurugenzi
wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya
mama ngojea katika hospital ya Kinyonga na ukarabati wa
wodi ya uzazi mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo
katika hafla fupi iliyofanyika jana Kilwa
Kivinje.
Meneja
Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya
ujenzi
wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama
wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali
ya
Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha
uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya
cha
Kilwa Masoko. Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary
(wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili
kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh.
Vedasto
Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia
chama
cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza
kulia).
Mbunge
wa Kilwa Kusini kupitia chama cha
CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa
Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara
baada
ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa
kilwa.
Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya
wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba
cha
uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi
uliosainiwa
kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za
serikali za kuboresha huduma za afya.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia