Muimbaji wa muziki wa Kizazi kipya kutokea Kenya aitwae Kigoto,
ametupa lawama kwa hit maker wa Shikorobo Shetta akimtuhumu kumuibia
wimbo wa Kerewa.
Kigoto ambaye jina lake halisi ni Ali Mbonde, amesema mara ya kwanza alikutana na Shetta mjini Mombasa alipokwenda kufanya show.
Anaendelea kusema kuwa baada ya kufanikiwa kuonanana nae kwa msaada
wa muongozaji wa Video nchini humo Hamza Omary, alimshawishi Baba Qailah
ili wafanye wimbo wa pamoja.
Kigoto anasema shetta alimkubalia na mwisho wa siku wakaelekea Studio pamoja.
Anashuka zaidi kwa kusema siku hiyo Shetta alidai amechoka ndipo
Kigoto akaamua kumuandikia mashairi ambayo ameyasikia kwenye Hit ya
Kerewa aliyoifanya na Diamond.
chanzo:blog ya wananchi