Waziri
Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo wakati alipotoa taarifa ya
serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa TPA, TRA,
Wizara ya Uchukuzi na TRL. kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni
Sefue.
Waziri
Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wa kwa utulivua
wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari , Kalia ni
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza
Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa
makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.
Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya
ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali
kinyume cha utaratibu.
Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo
ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai
2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji
kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba
2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu
hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote
inayochukuliwa.
Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea
malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya
Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri
panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.
Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote
kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile
kwa manufaa ya wachache.
Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:-
1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka
Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa
na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015.
2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena
hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu
nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na
utaratibu.
1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD)
(i) Happygod Naftari
(ii) Juma Zaar
(iii) Steven Naftari Mtui
(iv) Titi Ligalwike
(v) Lydia Prosper Kimaro
(vi) Mkango Alli
(vii) John Elisante
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.
2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya
makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni
wahusika wakuu.
1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari
Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi
Co-operate Services.
3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha.
4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha.
5. James Kimwomwa.
Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa
wafuatao:-
1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka.
2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.
Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia
TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi
Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.
Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na
atapangiwa kazi nyingine.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia