MWANA FA AFUNIKA KATIKA ONYESHO LA HAFLA YA MIAKA 250 YA HENNESSY

Mwana FA akiimbaKulikuwa na muziki poa kutoka kwa Dj
Madam Ritha Paulsen akiwa na Mwana FA pamoja na Mmiliki wa Oasis Baa, Nuru mosha
Akiendelea kuimba huku akiwa na chupa yake ya Hennessy
Mheshimiwa Zitto pia alikuwapo
Chupa ya Hennessy 250 Collectors blend iliyotengenezwa maalum kusherekea miaka 250 ya kinywaji hicho.
Kwa ndani kulikuwa na eneo lilikowekwa picha mbalimbali kuhusiana na historia ya kinywaji hicho
Wageni waliojumuika pamoja siku hiyo
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amezikonga nyoyo za mashabiki wake kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 250 ya kinywaji cha Hennessy yaliyofanyika katika baa ya Oasis Masaki.




Mwana Fa alianza kuimba majira ya saa nne ambapo alianza kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali zilizowahi kutamba kama vile, Mimi na Mabinti pamoja na nyinginezo za zamani.

Baada ya kumaliza nyimbo hizo za miaka ya nyuma akaanza kuimba nyimbo zake za sasa ukiwamo ule wa Mfalme na nyinginezo mpya.

Watu wengi walihudhuria hafla hiyo ya maadhimisho ya kinywaji hicho iliyoenda sambamba na maonesho ya michoro mbalimbali kuhusianana historia ya kinywjai hicho ambacho asili yake ni Ufaransa.

Pia watoa burudani mbalimbali kama vile kundi la Mosaic Collective pamoja na Mac Band walitoa burudani.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo, mratibu wa maadhimisho hayo ambae pia ni mmiliki wa baa ya Oasis Nuru Mosha alisema kuwa kinywaji hicho kimekuwa karibu zaidi na sanaa ya Tanzania kwa ujumla mbali na kufanya biashara.

Mosha alisema kuwa kwa kuwa mwanzilishi wa kinywaji hicho alikuwa ni mtu mpenda sanaa hasa aiwa anajishughulisha na sanaa ya uchoraji na hivyo wageni wanaotembelea michoro hiyo wanapata kufahamu kiundani zaidi historia ya kinywaji pia.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post