Mmoja
kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Charles Mlay akizungumza juzi kwenye
mkutano wa wachimbaji wadogo Marema kuhusiana na maandamano ya amani
kupinga migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.
WACHIMBAJI
wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, wanatarajia kuandamana hadi kwa mkuu wa mkoa huo, wakipinga
kusimamishwa kazi migodi yao 19 inayopakana na TanzaniteOne.
Wachimbaji
hao wanatarajia kuandamana kwa amani mapema mwezi ujao na watamuandikia barua
mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera ili ayapokee maandamano hayo wakipinga
kunyanyaswa na kusimamishwa migodi yao 19.
Mmoja kati
ya wachimbaji hao Charles Mlay akizungumza juzi kwenye mkutano wa chama cha
wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Marema, alisema wachimbaji wamekuwa
wananyimwa haki zao bila sababu ya msingi.
“Hakuna mtu
aliye juu ya sheria kila wakati wachimbaji wadogo wananyanyasika kwa kunyimwa
haki zao wakati wanachimba kihalali hivyo ni bora kufanya maandamano ya amani
yatakayoeleza hisia zetu,” alisema Mlay.
Makamu
Mwenyekiti wa Marema Wariamangi Sumari alisema maandamano hayo ya amani
yatajumuisha wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wakazi wote wa Mirerani
kwani maisha yao yanategemea madini ya Tanzanite.
“Maandamano
hayo yatakuwa ya halali kabisa kwani tutaomba kibali kwa mkuu wa polisi wa
wilaya (OCD) na kumtaarifu mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa aje hapa Mirerani kwa
ajili ya kupokea maandamano hayo,” alisema Sumari.
Omary
Mandari alisema kitendo cha migodi hiyo 19 kusimamishwa kufanya kazi
kimewaathiri watu wengi kiuchumi, kwani familia nyingi za wachimbaji hao
zinategemea kuishi ila kutokana na hali hiyo, sasa wanaishi kwa wakati mgumu.
“Tutaandamana
kwa amani kuanzia shamba la Maro na kuzungukia kwenye baadhi ya barabara za
Mirerani hadi getini mnadani, kwa lengo la kuonyesha ulimwengu kuwa tunapinga
migodi yetu 19 kusimamishwa,” alisema Mandari.
Naye, katibu
wa Marema Abubakari Madiwa alisema azimio hilo la kuandamana kwa wachimbaji hao
wadogo linaandaliwa ipasavyo ikiwemo kamati ndogo itakayoratibu mpango wote
hadi kufanikisha maandamano hayo ya amani.
Zephania
Joseph alisema haki ya wachimbaji wadogo haiombwi inadaiwa, hivyo huu ni wakati
muafaka wa kuungana kwa wachimbaji hao kufanya maandamano ya amani ili
kufikisha kilio cha kwa migodi yao 19 kusimamishwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia