Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.
Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Makusaro Tesha wa Kupatana wakizungumza na wadau wa KUPATANA
Wafanyakazi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja,
Mama Kupatana akisalimiana na mmoja wa wadau wa KUPATANA.
Wafanyakazi wa KUPATANA wakiwa katika tafrija hiyo ya kufunga mwaka 2015
Msimamizi wa shughuli za Kupata, Ezekiel Alex akizungumza kuhusiana na jumuiko hilo.
Mkuu wa huduma kwa wateja, Neema Mwakalonge akizungumza.
Msimamizi wa bidhaa za 'Real Estate' Liberator Wyson akizungumza.
Msimamizi wa bidhaa mchanganyiko, Jesca Mathew nae akitoa salamu
Muda wa maanjumati ulifika na wateja pamoja na wafanyakazi wa Kupatana.com walijumuika katika mlo huo.
Wafanyakazi wa Kupatana.com na wateja wao walikula na kunywa
Burudani ya mziki ilikuwepo ya kukata na shoka.
**************
Kupatana.com ni website ya
matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania.
Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa
kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.
Dhumuni la website ya
Kupatana.com ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa za bidhaa ambazo zinauzwa
ikiwemo magari, samani, nyumba, vifaa vya umeme pamoja na nguo au
bidhaa binafsi. Lengo ni kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa zao. Katika hili, hadi sasa Kupatana.com
imefanikiwa kuwa soko kubwa kabisa la bidhaa mtandaoni.
Hadi sasa, tunatembelewa
na watu wanaozidi 67,000 kwa siku. Kwa kutumia mtandao huu, muuzaji anaweza
kupata mafanikio Zaidi kwa kufikisha taarifa ya bidhaa alizonazo nje ya eneo
alilopo bila gharama yoyote.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko
wa mtandao wa Kupatana.com Bwana Makusaro Tesha katika hafla ya chakula cha
jioni ambayo ilihudhuriwa na wafanyakazi na baadhi ya wateja wa Kupatana.com …
Vilevile katika hafla hiyo Mr. Tesha alitoa wito kwa vijana na wajasiriamali
kuchukua fursa na kuutumia vizuri mtandao wa Kupatana kwani hauna gharama na
unawafikia wanunuzi wengi. Alisema, “jambo la kwanza ni kupakua (download)
application ya kupatana kwa kupitia Google play store. Ukiwa na app ya Kupatana
na kuitumia inavyopaswa ni sawa na kuwa na duka lako wakati wote”.
Vilevile baadhi ya wateja
waliohudhuria hafla hiyo walisema kuwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza
mauzo kwa kutumia mtandao huu. Mmojawapo wa wateja hao Bwana Mohammed Waqas wa
Jazmak Motors alisema toka waanze kutangaza magari yao kwenye mtandao wa Kupatana
wamekuwa wakipata wateja wengi hata kutoka nchi za jirani ikiwemo Malawi na
Zambia.