BREAKING NEWS

Saturday, January 16, 2016

KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHILISHWA.

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.

Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae kuahilishwa kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea kusikilizwa kuanzia majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na moja jioni.
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani) akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema)

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates