Hii ni
Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo
hili kwa upande kwa Kushoto.
Eneo hili wakazi
wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia
picha
Hii ni njia ya
kuelekea Pangoni
Ukiwa Juu ndani ya
Pango utaona hivi
Mmoja wa
wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo
hilo.
Watu wengi
wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya
utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za
Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii
wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa
fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa
mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa
jiji.
Irente View Point
inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani
Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa
wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine
walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa
wakati wa sikukuu za Christmas
Eneo hili lina
urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona
maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi
wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona
Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.
Jinsi ya kufikia
ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh
3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh
3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh
2,000.
(Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)
(Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)