Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh.
Shy-Rose Bhanji, (kushoto), akipeana mikono na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh.Eugene Kayihura ofisini
kwa balozi Masaki jijini Dar es Salaam, Jumatano Januari 13, 2016. Mh. Bhanji
alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye nchi yake
ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan
Said)
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, (kushoto),
akiwa na mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura kwenye
ofisi ya Balozi, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatamo Januari 13, 2016. Mh.
Bhanji alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye
nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), tawi la
Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura, ofisini kwa Balozi, Masaki jijini Dar es
Salaam, leo Jumatano Januari 13, 2016.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano
wao, Mh. Bhanji alsiema, Rwanda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kama ilivyo kwa Tanzania, na Bunge la Afrika Mashariki linaundwa na
wabunge kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya
na Uganda, hivyo aliona umuhimu wa kwenda kumtakia heri ya mwaka mpya balozi
huyo wa Rwanda.
Naye Balozi wa Rwanfa hapa nchini, Mh. Kaihura, alimshukuru
mbunge huyo kwa kumtembelea ofisini kwake na kumtakia heri ya mwaka mpya, na
kumuhakikishia Rwanda ambayo ni mwanachama wa Jumuiya itaendelea kushirikiana
na nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kujenga Afrika Mashariki iliyo na ustawi
wa hali ya juu na ushirikiano uliotukuka
Mh. Bhanji akizungumza na waandishi wa habari
Mh. Bhanji na balozi Mh. Kaihura wakiwa kwenye mazungumzo
Mh. Balozi Kaihura akizungumza na waandishi wa habari
Mh. Bhanji akiweka saini kitabu cha wageni ofisini kwa balozi Kaihura
Mh. Balozi Kaihura akimsindikiza mgeni wake Mh. Bhanji
Mh. Balozi Kaihura, akimuonyesha umbo la kitamaduni lililobuniwa nchini Rwanda likionyesha rangi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki