Askari wa Bunge wakiwa wamebeba
jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara,
Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada
ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam
leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere
Msasani kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi
yatakayofanyika keshokutwa.
Mwili huo ukiingizwa kwenye gari
maalumu katika uwanja huo.
Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana
jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa
marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere
akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani
hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na
mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani
hapo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia