ngoma za asili zikiwa zinatumbuiza katika uwanja wa KIA mara baada ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutua na ndege uwanjani hapo
baadhi ya wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki Magufuli
Na Woinde
Shizza,Arusha
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi ya Tanzania ni tajiri na inarasilimali nyingi ,ila baadhi
ya matajiri ambao ni mafisadi ndio wanasababisha nchi yetu kuonekana
maskini hivyo amehaidi kula nao sahani
moja.
Aliyasema
hayo leo wakati akiongea na wananchi wa mkoa wa Arusha waliojitokeza barabarani kumpokea huku wakimuomba aendelee kutumbua majipu.
Alisema kuwa
nchi ya Tanzania inarasilimali nyingi ila kunabaadhi ya matajiri ambao wanapenda
kujilimbikizia fedha wamekuwa wakifanya ufisadi na kusababisha baadhi ya
wananchi kuendelea kuwa maskini pamoja
na nchi yetu kuonekana maskini .
“nasema hivi
kuanzia sasa nipo tayari kulala mbele na mafisadi wote na pia nawapa onyo kali
wale walimu ambao bado wanatoza ada mashuleni iwapo nitagundua mwalimu
yeyote anaetoza ela nahaidi ivi nitalala
nae mbale ,na katika hili sitalifanyia
masiara ata kidogo”alisema Magufuli
Aidha
aliwaambia wananchi kuwa kuanzia sasa elimu ni bure kuanzia shule ya msingi adi
sekondari na serekali imeshaweka mipango hiyo tayari na imeanza kutumika.
Magufuli
aliwasihi wananchi wa mkoa wa arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya
kazi na kusema kuwa wakati wa kampeni umeisha , mambo ya siasa yameisha sasa
ivi ni wakati wa kufanya kazi tu na sio kitu kingine.
“nasema ivi
sasa ivii ni wakati wa kufanya kazi kama
nitaendelea kutumbua majipu kila mahali na sitawaonea huruma mtu yeyote
mimi kazi yangu kubwa ni kufanya kazi tu na wananchi napenda kuwambia fanyeni
kazi kwani hapa ni kazi tu”alisema Magufuli.
Alisema yote
aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla ikiwemo
ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule
za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Dkt. Magufuli
ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote
wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.
Rais Magufuli
amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila
yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka
watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.
Rais
magufuli alipokelewa na mamia ya
wananchi mbalimbali ambao walijitokeza
barabarani ambapo pindi tu alipotoka katika kiwanja cha kia wananchi walikuwa
wemejitokeza wengi mpaka ikamlazimu kufika
katika baadhi ya maeneo na msafara wake kusimama ili wananchi waongee
nae,sehemu ambazo aliweza kusimama ni pamoja na kikatiti ,usa river pamoja na
Tengeru .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia