Zaidi
wa Wanafunzi 400 wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi katika Manispaa
ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamenufaika na msaada wa vifaa vya elimu vyenye
thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Kumi ili kuwawezesha hao kupata elimu.
Msaada huo umetolewa na Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika Mazingira Magumu na hatarishi cha Shaloom Care House kilichopo
katika Manispaa hiyo.
Mratibu wa Kituo hicho Msafiri Wana amebainisha
kwamba wanafunzi 221 wa shule za Msingi na wanafunzi 187 wa shule za Sekondari,
wamenufaika na msaada huo ambao ni pamoja na madaftari, kalamu na sare za shule
ambapo thamani yake ni shilingi Milioni Kumi na Laki Tano.
Baadhi ya wanafunzi waliopokea msaada huo wametoa
shukrani zao kwa Kituo hicho ambapo pia wamewasihi wanafunzi wengine ambao
wazazi ama walezi wao hawana uwezo wa kuwahudumia mahitaji ya kielimu, kufika
katika kituo hicho ili wapate usaidizi huo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa
Mulongo amewataka Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari pamoja na Maafisa Elimu kusimamia
vema matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni Mia Tisa Tisini na Tisa, Laki
Tatu na Elfu sabini na Sita zilizotolewa na serikali katika Mkoa wa Mwanza kwa mwezi
huu ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake ya kutoa elimu bure nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia