Rais Dk. John Magufuli leo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo kesho atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha (TMA), Monduli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, alisema Dk. Magufuli atawasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na amewaomba wananchi kujitokeza kumpokea.
"Nawaomba sana wananchi wa Mkoa wetu kw amara ya kwanza tangu awe rais, ndio anakuja Mkoani kwetu, tujitokeze kumpokea,"alisema.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha TMA Meja Jenerali PP Masao, Dk. Magufuli atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi la 57/15.
Alisema Dk. Magufuli atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi hilo, katika sherehe zitakazoanza saa mbili asubuhi chuoni hapo.
Meja Jenerali Masao alisema wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Dk. Magufuli ambaye pia ni Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, kufika mkoani Arusha na pia kutunuku kamisheni, baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo Oktoba, mwaka jana.
Katika hatua nyingine, wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha, zinazokabiliwa na tatizo la ugonjwa wa kipindupindu, wamewasilisha taarifa ya hatua iliyofikiwa katika kukabiliana na janga hilo, inayoonyesha kuwa ugonjwa huo sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na uko mbioni kumalizika kabisa.
Wakuu hao ambao ni Fadhili Nkurlu wa wilaya ya Arusha na Ernest Kahindi wa Longido, walisema kwa sasa katika maeneo yao, hakuna wagonjwa wapya wa kipindupindu na wameendelea kuwataka wananchi kuendelea kuzingatia kamuni za usafi.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia