WAZIRI WA AFYAMAENDELEO YA JAMII JINSIA WATOTO NA WAZEE ATEMBELEA ZAHANATI YA MPINGA SONGEA
Posted by
woinde
on
Thursday, January 14, 2016
in
Habari
MATUKIO
|
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo.
Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa Bima ya Afya.
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
|
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi |
|
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao |
|
Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya, kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi |
|
Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia