Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo wakiwa katika tafrija ya ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema wa mwishoni wa wiki iliyopita |
Mkurungezi wa Tigo kanda ya kaskazini Bw.George Lugata akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema mwishoni wa wiki iliyopita |
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye tafrija ya kufungua duka la Tigo same wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mh Evagry Keiya mapema mwishoni wa wiki iliyopita |
Kampuni
ya simu ya Tigo imefungua duka jipya la same ambalo limepunguza adha kwa wateja wa
kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kaskazini Bw.George Lugata alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.
"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika
eneo la Same ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na
wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa
kutumia simu za mkononi"Alisema Lugata
Aliongeza kuwa ufunguzi huo unaendana na kuboresha muonekano wa duka hili kuwa wa kisasa
Lugata alisema kuwa duka hilo linalopatikana katika mtaa wa shule linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.
Kwa upande wa katibu wa mkuu wa wilaya ya same Mhe. Evagry Keiya alipongeza hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya same .