Mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Chama Cha Mapinduzi ya Uhuru,Mzalendo na Burudani mkoani Arusha Shaaban Mdoe kushoto akikabidhiwa fomu ya kuwania kiti cha ukatibu uenezi mkoa wa Arusha kutoka kwa katibu msaidizi mkuu wa mkoa Omar Billal.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mwanahabari Shaaban Mdoe akionyesha fomu ya kuwania nafasi ya uenezi mkoa wa Arusha kwa wanahabari baada ya kuchukua fomu hiyo kutoka kwa katibu msaidizi mkuu mkoa Omar Billal leo ofisini,
Mwanahabari Mdoe akipokea maelekezo ya ujazaji wa fomu hiyo kutoka kwa katibu msaidizi mkuu wa mkoa wa Arusha Omara Billal kabla ya kukabidhiwa.
Mwanahabari Mdoe akisubiria kukabidhiwa fomu ya kuwania nafasi ya ukatibu uenezi kutoka kwa katibu msaidizi mkuu wa mkoa Omar Billal.
Mwanahabari Mdoe kulia na mwana mwanahabari mwandamizi kutoka kampuni ya New Habari Corporation mkoani Arusha Abraham Gwandu akisoma majina ya wanachama wa CCM walojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo mdogo
Mwanahabari Mdoe akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali mkoani Arusha muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya katibu uenezo mkoa wa Arusha ili kuelezea sera zake