Picha maktaba ikionyesha wananchi jamii ya kimasai wakiwa wanacheza mpira
Na woinde shizza,Arusha
Na woinde shizza,Arusha
Chama cha soka wilaya ya Mondoli (MODFA),kinatarajia kufanya uchaguzi Mkuu Mwezi wa pili mwaka huu (2016), ili kupata uongozi kwa nafasi nane zinazowaniwa ili kupata uongozi utakao kiendesha chama hicho kwa miaka mitatu.
Katibu Mkuu wa Chama cha soka wilayani humo Twaha Kibayasi, alisema kuwa taratibu kamilihazija kamilika japo mambo yanaenda vizuri na nafasi nane ndizo zinazowaniwa katika uchaguzi huo.
Nafasi zitakazo waniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Muweka Hazina, Mjumbe wa mkutano Mkuu, Mwakilishi wa Vilabu na Wajumbe watatu wa kamati tendaji.
“Zoezi la uchukuajiwa wa fomu bado halijaanza na pindi taratibu zitakapo kamilika tutawatangazia lasmi ikiwa pamoja na ada ya kila nafasi itakayo tangazwa, cha msingi ni kuwaomba wajitokeze na wawe tayari kugombea nafasi hizo” alisema Kibayasi
Kwa mujibu wa katiba ya MODFA mtanzania yeyote mwenye Sifa zitakazo ainishwa ikiwa pamoja na elimu ya sekondari na kuendelea anafaa kugombea nafasi yoyote.
“Sio sifa hizo pekee Pia asiyewahi kushitakiwa kwa kosa lolote na kufungwa na awe mpenda michezo ndio sifa mojawapo itakayoangaliwa maana watu wanapenda kuleta siasa kwenye michezo na mwisho kuhalibu soka” aliongeza kusema Kibayasi.
Kibayasi alisema kuwa mara baada ya mwaka mpya Kamati tendaji ya MODFA inatarajia kukaa pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwepo juu ya kuandaa ligi ya Wilaya hiyo inayo suasua ili kupata bingwa atakaye iwakilisha Monduri katika Ligi ya Mkoa wa Arusha inayotarajia kuanza mapema mwezi januari.
Uchaguzi huo umehairishwa zaidi ya mara mbili kutokana na sababu mabali mbali ikiwemo watu kutojitokeza kugombea nafasi zilizotangazwa, uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika mwezi wa tano mwaka uliopita (2015).
Kibayasi Aliongeza kuwa kwa sasa wasipojitokeza watafanya uchaguzi kwa nafasi ambazo zitapata wagombea na pia wataandaa uchaguzi mdogo hadi wajaze nafasi zote kulingana na taratibu na sheria za MODFA