Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara (wapili
kulia) akitoa maekekezo kwa Viongozi wa TTCL katika ziara yake Mkoani
Mtwara juzi
Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya
TTCL, Prof. Tolly Mbwette na Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha
Kazaura Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha
Kazaura (wa kwanza kushoto) akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara mkoani Mtwara
Mazungumzo kati ya Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika mkutano na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara alipofanya ziara
yake
SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za kuilipa kampuni ya
Bharti Airtel ili kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika Kampuni ya Simu
Tanzania, TTCL.
Uamuzi huo unaotarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi huu
utaiwezesha TTCL kurejesha hisa zake 35% zilizonunuliwa na Airel mwaka 2001
na kuifanya Bharti Airtel kuwa mbia mwenza katika Kampuni hiyo. Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa ametangaza uamuzi huo
Jumatatu hii Mkoani Mtwara alipotembelea Ofisi za TTCL Mkoa wa Mtwara,
kukagua mitambo na miundo mbinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
"Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania na wadau wote wa
TTCL kuhusu kuondoka kwa mbia mwenza Kampuni ya Bharti Airtel. Ubia huu wa
TTCL na Bharti Airtel utahitimishwa Rasmi kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Tumefanya majadiliano ya kutosha, tumekubaliana kuwa Serikali iilipe
Bharti Airtel sh bilioni 14.9 ili kurejesha hisa za 35% za TTCL na kuifanya
Kampuni hii ya TTCL kuwa mali ya Umma kwa 100%.
Tutatumia fedha za Mapato ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kukamilisha
utaratibu huu. Naiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kufanya kazi kwa bidii
na Ufanisi Mkubwa na kusimamia kikamilifu shughuki za TTCL ili kutimiza
jukumu lake kwa Umma. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof.
Tolly Mbwette amesema, kukamilika kwa mchakato huu ni hatua muhimu sana kwa
Uhai na ufanisi wa TTCL na kusisitiza kuwa, mpango wa mageuzi ya kibiashara
wa kampuni hiyo sasa utatekelezeka kwa kasi kubwa baada ya hatua hii.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura amesema, jitihada kubwa
za TTCL sasa zitaelekezwa katika kuboresha huduma kwa kutumia fedha za
ndani na Mikopo ya wadau wa kibiashara ili kuiwezesha kampuni kuendelea
kuwa kiongozi katika utoaji wa huduma bora na nafuu katika soko la
Mawasiliano nchini.
Hivi karibuni, TTCL imezindua huduma za Mtandao wenye kasi zaidi wa 4G LTE
na kuimarisha ubora wa huduma zake za data na sauti.
Aidha, TTCL na Benki ya TIB zimeingia makubaliano ya mkopo wa fedha na
dhamana za Benki utakaoiwezesha TTCL kupata fedha dola za Marekali milioni
329 ili kuingiza mitambo mipya ya kisasa itakayo boresha huduma zake ikiwa
ni pamoja na kuanzisha huduma ya miamala ya fedha kwa njia ya mtandao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia