MWANDISHI UHURU AJITOSA UENEZI MKOA


Na Woinde shizza,libeneke blog Arusha
MWANDISHI wa habari wa magazetila Uhuru,Mzalendo na Burudani mkoani
Arusha Shaaban Mdoe amejitokezakuwania  nafasi ya ukatibu wenezi wa
CCMmkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mnamo
Januari 28mwaka huu ili kuziba nafasi zilizo wazi kutokana na sababu
mbalimbali.
Mdoe ambaye amewahi kuwamjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Arusha na
mjumbe wa kamati mbalimbali zamaadhimisho ya sherehe mbalimbali za
chama amesema amejitokeza kuwania nafasihiyo kutokana na msukumo wa
fani yake,uzoefu katika chama na kazi mbalimbali zachama kupitia
taaluma yake ya habari.
Akizungumza na gazeti hilialisema kutokana na nia yake hiyo
kesho(leo)atachukua fomu ya kuwania nafasihiyo katika ofisi kuu ya CCM
mkoa wa Arusha ambapo pia atapata nafasi ya kuelezamikakati yake pindi
jina lake litakaporejeshwa na vikao mbalimbali vya chama.
Alisema sasa wakati umefikawa chama kupata viongozi wake katika baadhi
ya nafasi kulingana na taalumakwakua ni jambo la muhimu taalumu
kuzingatiwa katika kushika nyadhfa hizokwakua itasaidia katika
utendaji kazi wake na kuleta mafanikio.
Alisema kupitia taalumayake ya habari ameweza kufanya mambo mengi
ikiwemo kuwaunganisha waandishi wahabari na vyombo mbalimbali wa mkoa
wa Arusha katika kukitangaza chama jamboambalo anaamini pindi
atakapopewa ridhaa hiyo ataifanya kazi hiyo zaidi ya palealipofikia.
Mdoe anaeongozwa na kaulimbiu yake kuwa “Mshale unarudi porini”
akimaanisha nafasi ya uenezi inahitajitaaluma ya habari,mahusiano na
utendaji kazi wa kazi hiyo wakati wote na sikuwa na taaluma pekee bila
kuifanyia kazi.
“unajua ile dhana ya zamaniya uenezi kuwa ni ya kupanda jukwaani na
kutambulisha wageni imepitwa na wakatikinachohitajika kwasasa ni
kupata kiongozi wa nafasi hii mwenye kutenda kazihiyo kila wakati
kwani mimi ni mwandishi sizuiwi na kazi nyingine hivyo nikiwa
katikaziara za kujenga chama pia niko katika ajira yangu”alisema
Mdoe.Mbali na mdoe wenginewaliotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na
aliyewahi kuwa mwenyekiti waChadema Monduli Amani Silanga,aliyekuwa
katibu wa siasa na uenezi wilaya yaArusha Semi Kiondo na Ally Rajabu.
Nafasi hiyo ya ueneziiliachwa wazi na Isack Joseph aliyejiunga Chadema
ambapo chaguzi huo mdogo pia piaunajumuisha nafasi ya mwenyekiti wa
CCM mkoa kufuatia aliyekuwa mwenyekitiOnesmo Nangole kukihama chama.
Pia uchaguzi huo utafanyikakatika kiti cha uenyekiti wilaya ya Monduli
kufuatia aliyekuwa mwenyekitikujiunga Chadema,mchumi na mjumbe wa
halmashauri kuu ya taifa(NEC) wa wilayahiyo kufuatia aliyekuwa Mnec
Edward Lowasa kuhamia Chadema.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post