Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya piwa zilizokutwa kwenye
nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini Arusha katika operesheni ya
tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira
machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa
uuzaji wa pombe za kienyeji

Mgambo wa jiji Wakimwaga pombe za kienyeji aina ya piwa zilizokutwa kwenye
nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini Arusha katika operesheni ya
tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira
machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa
uuzaji wa pombe za kienyeji,

Wananchi wa Mtaa wa Matejo uliopo jijini Arusha wameiomba serikali
iwapatie mikopo ili waweze kufanya shughuli mbadala za kujiingizia
kipato badala kujishughulisha na uuzaji wa pombe haramu ambazo
zinadaiwa kuwa sababu mojawapo ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindu pindu
kutokana na mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wake.
Wananchi hao wakizungumza katika operesheni ya tokomeza kipindupindu
iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ,kwa kushirikiana na
Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya
kupikia pombe hizo aina ya piwa,dadi na chang`aa ambazo pia huathiri
afya za watu.
Ester Stephano Shaka ambaye ni Muuzaji wa pombe hizo na Wilfred
Lyakimu na walisema kuwa maisha yao yanategemea biashara ya pombe za
kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya
nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya
biashara mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.
“Tunategemea shughuli ya kupika na kuuza pombe za kienyeji kuendesha
maisha yetu ,serikali haiwezi kuwaajiri watu wote tunaiomba serikali
itutafutie shughuli mbadala kwani hapa ndio tunapata chakula na
mahitaji muhimu “ Alisema Wilfred
Mkazi wa Matejo Jovan George alisema kuwa kutokana na tatizo la ajira
limewapelekea watu wengi kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi
ya pombe hivyo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala .
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki
alisema kuwa uteketezaji wa pombe haramu ni moja kati ya jitihada
wanazozifanya katika utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani
kutokana na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi
hilo ni endelevu.
Alisema Ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini
tayari wananchi wameanza kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi
licha ya baadhi ya maeneo kukithiri kwa uchafu hivyo kukwamisha
jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.