BREAKING NEWS

Friday, January 22, 2016

WAMUOMBA MAGUFULI AWATATULIE TATIZO LA KIWANDA CHA MAFUTA KINACHO WACHAFULIA MAZINGIRA


 Rais Magufuli akiwa anaongea na wananchi wa eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha

Na Woinde Shizza,Arusha



Msafara wa Rais John pombe magufuli   uliokuwa ukielekea monduli  (jana) umesimamishwa na wananchi  katika eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha  ili kushinikiza kuta kero zao na changamoto zao ikiwemo kuwepo na  kiwanda cha mafuta  ya kupikia cha  Mount Meru   Mill  kinachodaiwa kuchafua mazingira na kuatharisha afnya za wakazi wa eneo hilo.



Wananchi hao ambao walijikusanya kuanzia mida ya saa mbili kamili asubui mbali na kumueleza rais huyo kero zao pia walitumia nafasi hiyo kumpongeza kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu yaliyopo  humu nchini.



Akiongea mbele ya rais mara baada ya kupewa nafasi  mmoja wa wanachi wa eneo hilo la mbauda  Dhabiti Abubakari alimuomba rais awasaidie kutatua tatizo la kiwanda hilo kutiririsha maji machafu ya kiwandani  kwani tatizo hilo ni baya na linawaaribia mazingira  na kuatarisha afya zao .



‘’musheshimiwa rais tunapenda utusaidie apa kwetu mbauda tuna kero kubwa inatusumbua kunahiki kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mount meru mill kimekuwa kinatiririsha maji machafu ya kiwandani huku nje ambapo wananchi wanaishi  , kiwanda hichi  hakijajenga mitaro  ya kupitisha maji machafu hivyo maji yote machafu yakitoka huko kiwandani yanaingia huku majumbani kwetu hivyo muheshimiwa tunaomba utusaidie hili tatizo kwani kiwanda hiki kipo ndani ya makazi ya watu sasa inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao wanacheza uku mitaani pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama kipindupindu maana maji haya ni machafu sana”alisema Dhabiti



Akijibu swala hilo Rais magufuli alisema kuwa amelisikia na aliwaagiza mamlaka ya usafi wa mazingira  nemc  kulifuatilia swala hili mara moja .

Aidha magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa jiji la Arusha kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwahaidi ataendelea kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa akifanya kampeni.



Alisema kuwa kipindi hiki akuja arusha kwa ajili ya kuongea na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi arusha kufanya mkutano mkubwa ambao pia atatumia mda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji la hilo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates