January 13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.
Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.