MTO WA MBU KUKUMBWA NA BAA LA NJAA




Mbunge wa Monduli ,Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na upepo
mkali uliotokea jana jioni katika kata ya mto wa mbu na kuharibu migomba

mingi  katika kata ya mto wa mbuhabari picha na woinde shizza,monduli
Wananchi wa Kata ya Mto wa Mbu iliyoko wilaya ya Monduli wako hatarini

kukumbwa na baa la njaa kutokana na upepo mkali uliotokea jana majira
ya saa kumi na moja jioni na kuangusha migomba ya ndizi ambayo
hutegemewa kama chakula kikuu na zao la biashara.





Wakulima hao walisema kuwa upepo huo mkali umeathiri mashamba makubwa
ya migomba hivyo wameiomba serikali ichukue hatua za haraka kunusuru
hali ngumu ya upatikanaji wa chakula itakayojitokeza siku zijazo.





Leyan Ngaboli na Moses Lengine ni wakulima wa ndizi wamesema kuwa
upepo huo utasababisha kusimama kwa biashara ya ndizi kwa kiasi
kikubwa kwani tayari wakulima wameanza kupata hasara kwa kulazimika
kuuza ndizi kwa bei ya chini ili zisiharibikie mashambani.






Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Kusumu Hassan  alisema kuwa
karibu kaya na hekari zimeathiriwa na upepo huo hivyo ameiomba
serikali isaidie wakulima hao waweze kurejea katika kilimo hicho
ambacho huzalisha ajira nyingi.







Kwa upande wake Mbunge wa Monduli Julius Kalanga aliyefanya ziara ya
kuwatembelea waathirika wa upepo huo amewataka wananchi kuchukua
tahadhari huku akiahidi kushirikiana na serikali kutafuta chakula cha
msaada kutoka serikalini ili kuwasaidia wakulima hao kwa kipindi
ambacho wanaanza upya kulima mashamba yao kwani zao hilo huchukua muda
mrefu.





"Nitazungumza na Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa mkoa tuangalie uwezekano wa
kupata chakula cha msaada ili kunusuru kaya zilizoathirika" Alisema
Kalanga







Kata ya Mto wa Mbu hutegemea kilimo cha matunda matunda kama zao la
biashara na chakula ambapo matunda mengi kutoka kata hiyo hupelekwa
katika masoko ya ndani nan je ya mkoa wa Arusha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post