Ticker

6/recent/ticker-posts

ATLANTIC MKWAWA RALLY OF IRINGA KUFANYIKA IRINGA TAREHE 21 NA 22 MWEZI HUU

 




Baadhi ya viongozi wa mashindano ya mbio za magari za Atlantic Mkwawa Rally of Iringa wakiongea na waandishi wa habari juu ya ubora wa mashindano hayo mwaka huu


Baadhi ya viongozi wa mashindano ya mbio za magari za Atlantic Mkwawa Rally of Iringa wakiongea na waandishi wa habari juu ya ubora wa mashindano hayo mwaka huu


  Na Fredy Mgunda,Iringa.


Mashindano ya mbio za magari yanatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi na Jumapili Mkoani iringa katika mashamba ya Mt Huwel Kwa kuhusisha jumla ya madereva 15 kutoka nchi mbalimbali.


 


Akizungumza na waandishi Wa habari Mkoani Iringa mwenyekiti wa IMSC Amjad Khan alisema mashindano hayo yatafanyika Kwa Siku mbili kuanzia tarehe 21na 22 Mwezi wa tano mwaka huu 2022 siku ya Jumamosi na Jumapili.


 


Khan alisema kuwa mashindano yamekuwa na msisimko mkubwa na mashabiki wengi wa Mkoa wa Iringa na nje ya Mkoa wa Iringa hivyo Wananchi wanatakiwa kuwa makini ili kuepusha ajali barabarani.


 


Alisema kuwa wanejipanga kila eneo kuhakikisha usalama wa barabarani unakuwepo kwa Wananchi na watazamaji wa mashindano hayo hivyo Wananchi wanatakiwa kujitokeza Kwa wingi kushangilia.


 


Khan alisema kuwa mashindano hayo mwaka huu yanajulikana kwa jina la Atlantic Mkwawa Rally of Iringa.


 


 


Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa mashindano hayo Hidaya Kamanga alisema kuwa eneo ambalo mashindano yatafanyika lina ukubwa wa kilometa 116 na kilometa 105 ndio ambazo zitatumika katika ushindani wa magari siku Hiyo.


 


Kamanga alisema kuwa wanawakaribisha Wananchi wote na wadau wa mashindano ya magari kwa kuwa usalama umeimalishwa Kwa kiasi kikubwa na upo chini ya jeshi la polis mkoa wa Iringa.


 


 


Alisema kuwa jeshi la polisi litatoa elimu Kwa Wananchi juu ya usalama barabarani wakati wa mashindano ya Atlantic Mkwawa Rally of Iringa Kwa lengo la kuepusha ajali zisitokee Kwa Wananchi.


 


Kamanga alisema kuwa Kwa upande usalama wa afya wamejipanga vizurii Kwa kuwa na madaktari wakati wote wa mashindano hayo Kwa ajili ya kuwatibu majeruhi kama wakitokea.


 


 


Alisema kuwa mashindano hayo ya mzunguko wa pili yatakuwa ya ushindani kweli kweli hivyo Wananchi wajitokeze kupata furaha siku Hiyo.

Post a Comment

0 Comments