Na Woinde Shizza , ARUSHA
Halmashauri za wilaya ya Monduli,longido na Arumeru zimetakiwa kufanya jitihada zaidi katika uchangiaji wa fedha zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya lishe ili kupunguza tatizo ya lishe duni kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Hayo ya mebainishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya lishe mkoa wa Arusha Mosses Mabula alipokuwa akiongea katika kikao cha kujadili mwenendo wa hali ya lishe ndani ya mkoa wa Arusha ambapo pamoja na mambo mengine ambapo walitakiwa kuhakikisha halmashauri zote zinachangia fedha kwa ajili ya lishe
Aidha alitoa msisitizo kwa kwa zile halimashauri ambazo hajifikia lengo kufanya hivyo mara mojo ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Alitaja mikakati ya kubadilisha hali ya lishe katika mkoa wa Arusha imewekwa ni kuhamasisha halmashauri ambazo hazijatekeleza mpango huo wa kuchangia na kutumia fedha za lishe kufanya hivyo ili mkoa uweze kurudi katika alama ya kijani.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia