Ticker

6/recent/ticker-posts

WAATHIRIKA WA VIRUS I VYA UKIMWI WASHAURIWA KUACHA A NA DHANA POTOFU

 Na.Elinipa Lupembe.

Waathirika wa virusi ya UKIMWI, wameshauriwa kuachana na imani potofu, zinazowasababisha kuacha, kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI - ARV. Rai hiyo imetolewa na wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Arusha, wa robo ya tatu mwaka wa fedha 2021/2022, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmasahuri hiyo.

Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo, Diwani wa Kata ya Kimnyaki Mhe. Eliakimu Marivey,  ameuliza nini mkakati wa halmashauti kwa watu wanoishi na virusi vya UKIMWI, na kuamua kuacha kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo, kutokana na imani potofu zinazotokana na mila na desturi.

Akijibu swali hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi ameweka wazi kuwa, serikali kupitia watalamu wa sekta zote, inaendelea kutoa elimu kwa jamii, juu ya umuhimu wa vidonge vya kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI, na kuwataka viongozi wa mila na wale wa dini kutoa elimu sahihi kwa waumini wao kuhusu matumizi ya dawa hizo.

“Mara nyingi watu wamekuwa wakisitisha matumizi ya Dawa za Magonjwa kama Pressure na UKIMWI kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuchoshwa na dawa hizo pamoja na imani potofu, badala yake wanatumia dawa za miti shamba, hali inayopelekea kufupisha Maisha yao, niwaombe viongozi wenzangu tushirikiane kuelemisha jamii katika maeneo yetu”. Amesema Msumi.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho cha Madiwani, wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa jamii na kuifanya agenda ya kudumu kwenye mikutano ya vijiji, lengo likiwa ni kuwaelisha jamii matumizi sahihi ya dawa za ARVs pamoja na umuhimu wa dawa hizo kwa maisha.

“Ninawashauri watu wenye maambukizi waendelee kutumia Dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi kwasababu kuacha kutumia dawa hizo ni kuhatarisha maisha ya mtu binafsi, pia na wale watakaobainika kutoa elimu isiyo sahihi serikali iwachukulie hatua za kisheria”. Amesema Mhe. Elinipa Laizer, Diwani Viti Maalum

Mkutano huo wa Baraza la Madiwani umejikita kujadili utekelezaji wa shughuli za halmashauri, ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kiseta, mapato na matumizi pamoja na shughuli za maendeleo ya jamii na  ustawi wa jamii zilizotekelezwa katika maeneo yote ndani ya Halmashauri katika kipindi cha robo ya tatu ya kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2022.



Post a Comment

0 Comments