Ticker

6/recent/ticker-posts

WATAWALA WAIOMBA SERIKALI KUUNDA BODI YAO.

 


 




Maafisa rasilimali watu na watawala zaidi ya 500 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakutana jijini Arusha kujadili namna ya kuunda bodi itakayowasidia katika kutatua changamoto zao pamoja na kuwa na chama kimoja kitakachobeba mlengo mzima watawala na rasilimali watu.



Akizungumza jijini Arusha kando ya mkutano huo,Katibu  mkuu wa taasisi ya utaalamu wa utawala Tanzania(APAT) iliyoandaa mkutano huo,Christopher Kabalika alisema kwa kuunda bodi hiyo itasaidia kuleta mlengo mmoja wa kiutendaji kazi.



Aidha Kabalika alisema kwa wao kama wasimamizi wa wafanyakazi hawana bodi itakayowasaidia kujadiliana na kuweka mambo sawa lakini kupitia mkutano huo wa siku tatu watajadili mambo mbalimbali ikwemo kuunda chama kimoja kitakachobeba mlengo. 


"Tunaiomba serikali kulichukulia jambo hilo la uundwaji wa bodi kwa makini na kuweza kuwa na bodi ambayo itasimamia sekta ya utawala katika kuweza kufanya kazi katika taasisi za umma na binafsi kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji kazi,"alisema Katibu huyo.


Kwa upande wake Afisa utumishi manispaa ya Temeke Bihaga Yogwa alieleza kuwa Kuna changamoto ya kutokuwa na bodi katika tasnia hiyo kwani wanakosa chombo kimoja kinachosimamia mambo yao lakini wakipata  bodi watakuwa imara na wenye nguvu zaidi katika kushughulika na masuala yao.


"Kwa kuunda bodi itatusaidia kuongeza mchango wetu katika utoaji wa huduma katika taasisi za serikali pamoja na binafsi kutokana matarajio ya chama ambacho kitakuwa imara kwenye kuangalia utendaji kazi wetu,"alisema.


Naye muhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Dkt Venance Shillingi alisema kuwa watakapo unganisha kada hizo mbili itawafanya wawe na nguvu itakayoshawishi serikali wawe na bodi ya kuwasimamia kwani wakiwa na bodi hiyo kada hizo zitakiwa na  ambavyo mpaka mtu awe navyo ndipo aweze kuwa afisa utumishi au afisa utawala.



“Kazi ya afisa utumishi sio kuajiri tu na kufukuza bali ni mtu pekee ambaye anaweza kufanya taasisi ikafanya vizuri kuliko kada nyingine  yoyote na hii itafanya afisa utumishi awe ni sehemu ya taasisi kwa kujua taasisi ina mikakati gani kwa miaka ijayo aweze kusaidiabkupata  wafanya wenye sifa stahiki ya kutekeleza hiyo mikakati,”Alisema Dkt Shillingi.



Alisema kuwa wakishaunganisha nguvu na kitu kimoja watakuwa na matawi mawili moja la maafisa utumishi na lingene utawala lakini kwa juu wanakuwa timu moja ili watakapokuwa na hoja yoyote waweze kusikilizwa.

Post a Comment

0 Comments