Na Woinde Shizza,ARUSHA
Imeelezwa kuwa kuonyesha mwanga ni dira ya demokrasia kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kumepelekea baaadhi ya migogoro kuibuka ndani ya vyama mbalimbali vya upinzani .
Akiongea na waandishi wa habari katibu wa itikadi na uwenezi taifa wa chama cha ADA-TADEA Zubery Mwinyi alisema kuwa ndani ya vyama vya upinzani kwa sasa kila mtu anajitokeleza kutaka kupata nafasi kwa kuwa kipindi hichi cha uongozi wa Rais Samia ni nafasi pekee ya kwenda kufanya siasa ambazo niza kweli na za utafiti
“kutokana na hayo ya kutaka nafasi ndani ya vyama ndio maana vyama vingi vinakuwa na migogoro na h ii ni ndio sababu wapo ya kuleta migogoro ndani ya vyama lakini tunasema kwamba Rais samia ametuonyesha dira kubwa katika siasa na ni mtu ambae anania ya kweli na nimkweli na ndio kitu ambacho kilikuwa kina subiriwa sana nawapinzani ndani ya Tanzania natuseme tu kwa sasa watanzania tumepata kiongozi ambaye ni mkweli na muwazi na tunaamini ataifikisha nchi yetu mbali”alibainisha Zuberi
Wakati huo huo katibu mwenezi huyo alisema kuwa chama hicho chama cha siasa cha ADA –TADEA kimepata viongozi wapya huku aliekuwa katibu mkuu John Shibuda akiwa amemwagwa katika uchaguzi uliofanyika June 28 katika ukumbi wa lego uliopo jijini Dar es salaam .
Alisema kuwa kwa upande wanafasi ya mwenyekiti imechukuliwa na yule yule Juma Ally Khatibu huku makamu wake kutoka Tanzania bara ni Zaituni Hokohoko ,makamu mwenyekiti Zanzibar ni Hassan Kijigoo,huku katibu mkuu akiwa Salehe Mhomamed Msumari ,naibu katibu kuu bara ni Georia’s Busungu ,Naibu katibu mkuu Zanzibar Hamis Mambo, nafasi ya katibu Mwenezi taifa Zuberi Mwinyi ,naibu katibu mwenezi Zanzibar Halima Abdaallah huku naibu katibu mwenezi bara akiwa Ireen Anatory.
Alibainisha viongozi hawa wapya waliochaguliwa ni vijana hivyo wamejipanga kukipambania chama chao ili kiwe chama cha kwanza cha upinzani kinachoongoza hapa nchini .
Aidha alibainisha baadhi ya mikakati waliokuwa nao kama chama ni kuakikisha kila mkoa chama kinatambulika na wananchi na kinasaidia kuboresha maendeleo ya wananchi