HOSEH APITA KWA KISHINDO KWA MARA NYINGINE UCHAGUZI WA URAIS TLS APITA KWA KURA ZAIDI YA 600




 Uchaguzi wa RAIS wa chama Cha Mawakili wa Tanganyika TLS umefanyika Leo ambapo Prof.Edward Hoseh ameibuka kidedea Kwa kupata kura 621 dhidi ya wapinzani wake Harold Sungusia aliyepata kura 380 na Jeremiah Mtobesya aliyepata kura 145.


Jumla ya wapiga kura wote walioshiriki kupiga kura katika uchaguzi huo kuwachagua makamu wa Rais na Rais ni 1150 pamoja na wajumbe wa komitii kutoka Kanda za chama hicho.

Akisoma matokeo hayo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Chals Rwechungura amesema kwamba uchuguzi huo umeenda Kwa haki na utaratibu wote Kwa kuzingatia uwazi na usawa.

Amewataja Kwa upande wa Makamu wa Rais walikuwa wagombea watatu ambapo alieshinda Gloria Kalabamu aliyepata kura 598 dhidi ya wapinzani wake Angela Mbonde aliypata kura 449 na aliyefuatia ni Nyachiringa Msalya aliyepata kura 99.



Akiongea Mara baada ya kuchaguliwa Prof.Hosea amesema kwamba atahakikisha atasimamia Uwazi,uwajibikaji na Uwekezaji kwa kuendeleza mambo yote Kwa uwazi Ili kufikia TLS ya uwekezaji.

Ambapo amewataka mawakili wazoefu waliokimbia chama kurudi na kukaa na vijana kuwafundisha maadili ya kazi pamoja na kuwapa uzoefu wa kazi

"Serikali iliyopo madarakani kipindi hichi ni nzuri ni vyema muitumie kuwekeza na sio kuwekeza kama chama bali hata sisi Kwa sisi mawakili wenyewe kwani TLS isiwe ni taasisi ya kuchukuwa fedha mifukoni mwa wanachama"alibainisha hoseh

Amesema kwamba muelekeo wa mawakili Kwa sasa ulenge kuwekeza katika vitega uchumi Kwa chama chao sanjari na kushirikiana kuweza kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi 


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post