Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT KAMATULA: NJOONI TUSHEREKEE SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI.

 



Na Sixmund Begashe


Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha kusherekea siku ya Makumbusho Duniani ili kujipatia uwelewa mpana wa mambo mbalimbali yanayo husu Urithi wa Utamaduni na Malikale uliohifadhiwa katika Makumbusho za Taifa.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt Gwakisa Kamatula, kwenye maandalizi ya mwisho ya Maadhimisho hayo Jijini Arusha na hasa wamejiandaa kikamilifu kupokea wageni wandani na nje ya Mkoa wa Arusha watakao udhuria Maadhimisho hayo.


Dkt Kamatula amesema Kituo chake kimejiandaa vyema kuonesha Nguvu ya Makumbusho kama Kaulimbiu ya Mwaka huu isemavyo katika kuhakikisha wanatoa huduma nzuri na bora kwa wageni wengi watakaokuja hasa wanaotokana na matokeo makubwa ya Filamu ya Royal Tour.


"Tunamshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutuonesha njia kupitia Filamu ya Royal Tour, Makumbusho ya Azimio la Arusha tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunaitendea haki heshma hii aliyo tupatia Mhe Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan hasa katika utoaji wa huduma zetu nk". Alisema Dkt Kamatula.


Dkt Kamatula ameongeza kuwa, Maadhimisho hayo yatapambwa na program za kielimu, Maonesho ya kudumu yaliyopo Makumbusho hiyo ya Azimio la Arusha na Maonesho ya Sanaa za Jukwaani kama Ngoma, Sarakasi, Musiki nk


Siku ya Makumbusho Duniani huadhimishwa Kila mwaka tarehe 18 Mei na Kaulimbiu ya Mwaka huu 2022 ni "Nguvu ya Makumbusho" hivyo Makumbusho ya Azimio la Arusha imeona iadhimishe  tarehe 20 ndani ya wiki husika ili kutoa nafasi kwa watu wengi hasa wanafunzi na Wanavyuo kuudhuria.

Post a Comment

0 Comments