Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJALIWA ARIDHISHWA NA JENGO LA UFUNDI TOWER LINALOJENGWA KATIKA CHUO CHA ATC

 


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa jengo la ufundi Tower katika chuo Cha ufundi Arusha (ATC) pamoja kusema kuwa  serikali inaendelea kufanya mapitio juu ya mkopo wa elimu ya juu kuona ni kwa namna gani mikopo hiyo itaweza kuwanufaisha na wanafunzi wanaosoma elimu ya kati.


Majaliwa ameyasema hayo leo Mei  24 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ufundi Tower ambapo alisema kuwa wamejikita sana kwenye shahada hivyo wakati umefika kuona ni namna gani  wataboresha  elimu ya kati ili vijana waweze kunufaika zaidi.


Ameeleza ameridika na ujenzi wa jengo hilo linalojuisha maabara, madarasa,pamoja na  clinic itayowahudumia watumishi, wanafunzi, na wananchi wa Arusha walio karibu na chuo hicho na kuahidi kuwa wataendelea kuleta fedha za ujenzi katika chuo hicho ili kupunguza changamoto ya mabweni.
Amefafanua serikali imetoa fedha za kutosha kwenye sekta ya elimu  kwanzia chekechea kwa wanafunzi wa kawaida wenye mahitaji maalum ambapo kwa sekondari wameanza kwa kujenga madarasa na sasa wanajenga mabweni ili kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa kike na wakiume.Kwa upande wake Kaimu mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt Musa Chacha alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulioanza Julai 2021 baada ya kupokea shilingi bilioni 1.449 kama ruzuku ya fedha za maendeleo kutoka serikali kuu kwaajili ya bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 428 ambapo lengo la mradi huo ni kuongeza fursa na idadi kwa wanafunzi wa kike. 
Alisema chuo kilitenga bilioni 1.036 ya mapato yake ya ndani mwaka wa fedha 2021/2022 ili kujenga kliniki ya tiba inayolenga kuboresha utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma programu ya vifaa tiba ambapo jengo la ghorofa tatu na sakafu moja ya chini lenye maabara, madarasa, ofisi na stoo ambalo limepewa jina la Ufundi Tower.

Post a Comment

0 Comments