Picha na maktaba
Na Woinde Shizza,ARUSHA
Kamati ya viongozi na wataalamu juu ya mgogoro wa Ardhi ya Tarafa ya Ngorongoro, Sale na Loliondo waliosilisha taarifa ya kukusanya mapendekezo kwa wananchi nakuwasilisha katika Ofisi ya Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano imesema kuwa inaamini serikali itatoa matokeo chanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa Ngorongorona utaleta suluhu katika utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo lenye kilometa za mraba 1500 bila kuathiri pande zote mbili
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo,Metui Sheudo wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha ambapo alisema mchakato huo wa mapendekezo ya wananchi umedumu kwa muda wa miezi mitatu ikiwa lengo ni kuwafikia wananchi katika kutoa mapendekezo yao.
Alisema kuwa wanatumatumaini kuwa mapendekezo hayo yatatolewa matokeo chanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa Ngorongoro na italeta suluhu katika utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo lenye kilometa za mraba 1500 bila kuathiri pande zote mbili
Metui alisema hatua hiyo ilifuata baada ya mchakato wa kuwashirikisha wananchi na makundi mbalimbali katika jamii kuwa hafifu katika kutatua mgogoro huo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nainoka noka,Edward Maura alisema wanaishukuru serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kwa kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kuunda kamati na kuandika mapendekezo ya jamii juu ya mwenendo wa changamoto zilizopo wilayani hapo.
Vilevile alisema japo matatizo yanawapelekewa kuhamishwa ni pamoja na zilezinazoelezwa ni wingi wa mifugo pamoja na ongezeko la watu kwa mujibu wa serikali pia wao kama Wananchi wameongeza matatizo mengine ikiwemo uwepo wa magugu vamizi
Alibainisha kupitia kamati iliyokuwa na wajumbe wa pande zote katika jamii wameikamilisha kazi kutokana na ushirikiano baina ya wananchi na wanakamati hali iliyoleta tija katika kuandika taarifa hiyo waliyoiwasilisha serikalini
Aidha walimshukuru waziri mkuu kwa kupokea taarifa hiyo japo kuwa tayari kulikuwa na maneno ya chini chini kuwa hata pokea na kuhiadi serikali kupitia Mbunge wa Ngorongoro kurudi kwa ajili ya majadiliano hivyo wanategemea taarifa hiyo kutoa mateokeo chanya.