Ticker

6/recent/ticker-posts

DC ARUSHA AMALIZA MGOMO WA DALADALA

 


Mkuu wa wilaya Ya Arusha Mh Saidi Mtanda amefika katika Stand kuu ya Dalala zinazofanya safari zake katika jiji la Arusha na kuzungumza na Madereva waliokuwa wameweka mgomo wa Kusafirisha abiria kutokana na kudai kuwa Bei ya Mafuta imepanda huku LATRA wakiwa wamepandisha kiasi cha shilingi 100 kwenye nauli lakini wao hawaruhusiwi kuchukua hiyo shilingi mia hadi baada ya kufika Mkuu wa Wilaya hiyo akiwa ameongozana na Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqe aliwasikiliza Madereva hao na kumuagiza Kiongozi wa LATRA Arusha aeleze hatua walizo chukua kwakuwa ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusiana na jambo hilo.

Kiongozi wa LATRA Arusha Akaeleza kuwa wao wameridhia ongezeko la shilingi 100 lianze kutumika kutokana na uhalisia uliopo kwa kuwa wao waliagiza bei hiyo ianze kutumika baada ya siku 14 ili wananchi waweze kupewa taarifa.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili DC Mtanda akatoa maelekezo ya Serikali ya kuwataka Madereva warudi barabarani kufanya kazi na kuridhia maamuzi ya LATRA kuruhusu ongezeko la shilingi mia moja kwa kila ruti wakati majadiliano mengine ya Viongozi yakiwa yanaendelea na kuwaeleza swala la bei ya mafuta ni swala la kidunia serikali kupitia kwa Rais na Waziri Mkuu hawalalali wanashughulika na swala hilo hivyo wawe watulivu mambo yatakuwa sawa.

Baada ya Maelekezo hayo hali ya Usafiri jijini Arusha imerejea kawaida na Daladala zimeanza kufanya kazi.


Post a Comment

0 Comments