Ticker

6/recent/ticker-posts

TEMDO WAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA HOSPITAL YA UHURU DODOMA


 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma imepokea Vifaa Tiba vyenye Thamani ya Shillingi Millioni Tano (5m) kutoka Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo  Tanzania (TEMDO) ya Arusha, ikiwa ni mchango wao  kwa huduma za jamii (Corporate Social Responsibility).

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi  Mkuu  wa TEMDO Mhandisi  Prof.  Frederick Kahimba alisema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya mchango wa Taasisi yao wa kurejesha huduma katika jamii.


Alitaja vitu ambavyo  wamevitoa ni pamoja na vitanda viwili vya kujifungulia wamama wajawazito , Vitanda Viwili vya Kulazia Wogonjwa Wodini , Vitanda Viwili vya Kufanyia Uchunguzi madaktari, pamoja na mihimili miwili ya Kutundukia Maji-Dawa (Drip stands). 

Mbali na hivyo pia Taasisi hiyo iliweza kukabidhi  kiteketezi cha taka hatarishi za hospital (biomedical waste incinerator) ambacho chenyewe kilinunuliwa na hospitali hiyo,na  kina uwezo wa kuchoma taka hatarishi kilo 100 kwa saa moja.

Alisema lengo kuu la kutengeneza Vifaa Tiba ni kuisaidia Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuagiza nje ya nchi vifaa vinavyoweza kutengenezwa na Taasisi Za ndani ya nchi, ambapo kuagiza huko kumekuwa kukitumia fedha nyingi za kigeni. 

Aidha pia alisema kuwa kutengeneza vifaa tiba hivyo vimesaidia kuongeza ajira za ndani na kurahisha upatikanaji wa bidhaa kirahisi na Kwa bei nafuu  huku akifafanua kuwa kwa sasa TEMDO inavifaa tiba  zaidi ya kumi na tano (15) vyenye ithibati ya TMDA.


Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa  halmashauri ya wilaya ya chamwino   Dr.Semistatus Mashimba aliipongeza taasisi hiyo Kwa kutengeneza vifaa hivyo na kusema kuwa vimesaidia sana kuipunguzia gharama serikali iliokuwa ikitumia kuagiza nje ya nchi.

Mhandisi Kahimba pia ametoa wito kwa wadau wa sekta ya afya na Serikali kwa ujumla kutumia Taasisi za ndani kama TEMDO ili waweze kutengenezewa vifaa Tiba vyenye ithibati ya TMDA, na vinavyokidhi mahitaji ya huduma za afya na hospitali zetu za Tanzania.

Post a Comment

0 Comments