Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA:VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI LINDENI NA KUZITUNZA MILA NA DESTU

 


Na Pamela Mollel,Arusha 

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan  amevitaka vyombo vya habari na wanahabari kuzilinda na kuzitunza Mila na desturi za kiafrika katika uhandishi wao ili kuepuka migongano.Mhe Raisi alisema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo kwa bara la Afrika kwa mara ya kwanza yamefanyika jijini Arusha.


Alisema kuwa waandishi ndio wanapaswa kuzilinda Mila na desturi za kiafrika kwa kuandika mema ya bara la Afrika 


"Katika Bara la Afrika tumebarikiwa sana vivutio mbalimbali tujivunie vyakwetu..wakati wengine wanazungumzia migogoro nyie zungumzieni amani "alisema Raisi Samia 


Pia amewataka waandishi wa habari kutumia vyema mitandao ya kijamii katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mila na desturi zetu


"Sasahivi unakuta watoto wa Kitanzania wanapiga picha za utupu wanaweka mitandaoni  je mila na desturi zetu zinaturuhusu kufanya hivyo?"alisema Raisi Samia Aidha aliwataka wanahabari kutambua kuwa pamoja na kuwa sheria zinawalinda lakini bado wanapaswa kujilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na wanahabari kutambua kuwa sheria ipo pale pale hivyo wafanye kazi kwa uungwana.
Kwa upande wake Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari  Nape Nnauye alisema kuwa vyombo vya habari na wanahabari watambue kuwa sheria zipo na wasimtie majaribuni .


"Wanahabari tambueni sheria zipo pale pale bado haijafanyiwa marekebisho hivyo basi msinitie majaribuni"alisema Nape


Naye Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania deodatus Balile alisema kuwa idadi ya waandishi waliouwawa imepungua ,huku akiiomba serikali ya Tanzania na nchi nyingine kuondoa Kodi ya VAT kwenye karatasi za kuchapisha magazetiKatika maadhimisho hayo washiriki kutoka  nchi 54  za Afrika wameweza kushiriki mkutano huo,huku Kauli mbiu yake ikiwa Ni uhandishi wa habari na Changamoto za kidigiti

Post a Comment

0 Comments