Ticker

6/recent/ticker-posts

Mahakama ya EACJ yapata msajiri mpya baada ya miaka sita

 

Msajili Msaidizi wa Mahakama ya Afrika Mashariki Christine Mutimura-Wekesa akila kiapo Cha utii jana jijini Arusha anayeshuhudia kiapo hicho ni Mwanasheria Mwandamizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Michel Ndayikengurukiye 

Na Woinde Shizza, ARUSHA

Mahakama ya haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ)hatimaye imepata naibu msajiri mpya baada ya kukaa kwa kipindi cha miaka sita bila kuwepo kwa mtendaji wa mahakama hiyo.


Akiongea kwenye hafla ya uapisho wa naibu msajiri huyo mpya ,iliyofanyika makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki,Rais wa Mahakama hiyo,Jaji Nestory Kayobeza alisema mahakama imeridhishwa na uteuzi wa naibu msajiri ambaye amekuwa ni wa pili tangu mwaka 2001 kuanzishwa kwa mahakama hiyo .


Jaji Kayobeza alisema kupatikana kwa naibu msajiri ,Christine Mutibura (45) ambaye uteuzi wake hufanywa na baraza la mawaziri wa EAC kutachochea ufanisi katika utendaji kazi wa mahakama hiyo kwani ni mzoefu wa mahakama na nchini kwake,Rwanda alikuwa ni mwendesha mashtaka wa serikali.


"Leo ni siku muhimu sana tumefurahi kupata naibu msajiri wa mahakama kwa sababu aliyekuwepo,Geraldine Umungwaneza alimaliza muda wake na mahakama kubaki bila mtendaji kwa muda mrefu kwa hiyo kupatikana kwa msajiri mpya kutasukuma mbele kazi za mahakama ili wananchi wa afrika mashariki wapate haki kwa haraka "alisema Jaji


Aidha jaji hiyo aliliomba baraza la mawaziri la EAC kuharakisha uteuzi wa msajiri kamili wa mahakama hiyo kwa kuzingatia kwamba mahakama hiyo tayari ina mahakama ya rufani hivyo kunahitajika mtendaji mkuu wa mahakama ili kuharakisha shughuli za mahakama zote mbili.


"Huyu ni mwanamke wa pili kutwaa nafasi hiyo ni mzoefu na anaelimu ya kutosha hata aliyemtangulia alikuwa ni mwanamke hivyo tunaimani kwamba wanawake wanafanya vizuri"alisema.


Kwa upande wake naibu msajiri ,Mutimura alishukuru kwa kuteuzi na kuapishwa kwake leo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili haki iweze kupatikama kwa uwazi na wananchi wa jumuiya hiyo waweze kuiamini mahakama hiyo.


Mutimura aliwaomba watendaji wa mahakama hiyo kumpa ushirikino ili kesi zinazoletwa ziweze kusikilizwa jwa haraka na kutolewa uamuzi kwa muda mwafaka ukizingatia kwamba mahakama hiyo ni kimbilio la wananchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Awali jaji mstaafu wa mahakama ya Rufaa ya EACJ na mahakama ya Rufaa ya Tanzania ,Edward Rutakangwa alisema mamlaka husika za jumuiya zilionelea umuhimu wa kuwa na mahakama hiyo ,hivyo kuwepo kwa watendaji wa mahakama kunaleta imani kwa wananchi katika upatikanaji wa haki.


Aliwataka wasajiri wa mahakama hiyo kuwa wasaidizi wakweli wamajaji na wajitahidi muda wote kusoma maamuzi yanayotolewa na mahakama ili kuisaidia mahakama kutenda kazi zake kwa uhuru zaidi.


Post a Comment

0 Comments