Ticker

6/recent/ticker-posts

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YAOKOA TRILIONI 10 ZA SERIKALI


Na Queen Lema

Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali imefanikiwa kuisaidia Serikali kuendesha mashauri ya madai na usuluishi na kuokoa kiasi cha Trilioni 10


Aidha mashauri hayo yamefanyika toka mwaka 2018 ambapo ofisi hiyo ilianzishwa.


Hayo yameelezwa na Bi Mary Makondo ambaye ni Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria hapo Jana wakati akifungua mafunzo ya mawakili wa Serikali, ambapo mafunzo hayo yameeandaliwa na ofisi ya wakili mkuu wa serikali


Makondo alisema kuwa ofisi hiyo toka kuanzishwa kwake imekuwa na msaada mkubwa sana kwa kuwa imekuwa ikileta usuluishi lakini hata suluhu juu ya madai mbalimbali


"Kwa kweli nataka niwaambie kuwa mmfenya jambo kubwa sana na mnastaili pongezo kubwa sana kwa sababu hizi fedha ni nyingi na  Kama hamkusimama ipasavyo  leo zingekuwa zimepotea"aliongeza Makondo


Katika hatua nyingine aliitaka ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi.kwa bidii sana sanjari na kusimamia maslahi ya taifa 


Aliwataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha kuwa wanaitumia elimu ambayo wataipata kwenye semina hiyo vema kwenye kazi zao ili kuendelea kuokoa zaidi.



Naye wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata amesema kuwa ofisi yake imekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya taifa hususani kwenye sekta ya uchumi


Akiongelea sakata hilo la kuokoa Trilioni 10 alisema kuwa wamepambana sana ili kuokoa kiasi hicho lakini endapo Kama wangeshindwa basi wangelazimika kulipa wadai 


Mbali na hayo alisema kuwa bado wanakabiliwa na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa watumishi wenye stadi maalumu


Nao washiriki wa semina hiyo walidai kuwa wanashukuru ofisi hiyo kuandaa mafunzo ya siku 4  ambapo elimu watakayoipata itawasaidia sana kuongeza ufanisi  katika kazi zao hasa za usuluishi

 

Post a Comment

0 Comments