Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Ashatu Kijaji pamoja na ujumbe wake Moja ya kifaa Cha mashine ya kuchakata miwa kinachotengenezwa na tahasisi hiyo juzi wakati waziri huyo alipotembelea kiwanda kicho kuona namna wanavyofanya
Na Woinde Shizza,ARUSHA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Ashatu Kijaji ameiagiza Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) kabla ya mwezi December wawe wamepeleka mitambo wa kuzalisha ,na kuchakata sukari kwa wananchi wanaoishi katika wilayani Kilombero ili kuweza kupunguza tatizo la upotevu wa miwa mingi inayolimwa na wananchi wa wilaya hiyo.
Aliyasema hayo wakati akiongea na wafanyakazi wa taasisi hiyo alipofanya ziara ya kuitembelea na kuona namna wanavyofanya kazi ambapo aliipongeza taasisi jinsi wanavyofanya kazi na kuwasihi waendelee kufanya kazi Kwa nguvu na Kwa Kasi zaidi
Alibainisha Wananchi wa sehemu za Kilombero ,mtibwa na sehemu zingine zinazolima zao la miwa ,mazao yao yamekuwa yakiharibikia sokoni kutokana na kukosa sehemu za kupeleka hivyo ni vyema wao kama Temdo ambao teyari wameshabuni na kutengeneza mtambo wa kutengeneza sukari wakaanza kupeleka mitambo hiyo katika sehemu izo Ili kuweza kuwapunguzia Wananchi adha ya kukosa sehemu ya kuuzia miwa yao.
"Ninajua sehemu ninyingi zinazolima miwa zinauhitaji ila nataka niwape kazi temdo adi ukifika mwezi December muwe mmeshawapelekea Wananchi wa mtibwa huo mtambo na baada ya Kilombero mpelekee na kwingine kama mtibwa na hata hapo Kilimanjaro kama Wananchi wanauitaji na icho kiwanda kinashidwa kuchukuwa na miwa yote ya Wananchi basi mnapeleka mashine ambayo itawasaidia Wananchi na uzuri wa mtambo huu mmesema unaweza kuwekwa hata nyumbani hauchukui sehemu kubwa naniwaambie tu Serikali inaela ya kutosha nyie kazi yenu ni kufanya kazi tu tena kwa kasi lazima tuwe na haraka maana tumechelewa tukimbie zaidi kwenda kwenye uzalishaji"alibainisha Kijaji
Alisema bainisha kuwa katika kipindi wizara hiyo ilivyokuwa ikiwakilisha bajeti yao bungeni ,wawakilishi wa wananchi bungeni walilalamika sana kuhusiana na miwa ya Wananchi kutupwa kutokana na viwanda vilivyopo kushidwa kuchakata miwa yao yote hivyo ni lazima tuwaonyeshe watanzania tupo na tunafanya kazi Kwa kuanza kupeleka mtambo huo Kilombero
"Miwa inatupwa Kwa nini kwa sababu viwanda haviwezi kuchakata miwa yote maana hii tunawazibiti wananchi wasilime miwa kwanini Kwa sababu hamna pakupeleka Sasa sisi Kama serikali tunakwenda kujibu matatizo ya Wananchi Kwa kuchukuwa ichi kiwandakili chotengenezwa na temdo cha milioni 500 tuwapelekee Wananchi wa pale Kilombero ,tunawawezesha vijana watanzania wamesoma waweze kuendesha waweze kusaga kuchakata miwa ya Wananchi na tutoe sukari ili tatizo la sukari liweze kuisha kabisa hapa nchini, wenzetu wa nje ya nchi mfano uganda ambapo tunaagiza sukari wameweza kwakuwa wameweza kwakuwa wamewezesha hivi viwanda vidogo vidogo na sisi Temdo , CAMARTEC ndio kazi yetu "alisema Kijaji
Aliwapongeza TEMDO Kwa kuanza kutengeneza vifaa tiba na kuwaahidi kuwa katika kutatua tatizo lao la kukosa wateja wa vitanda vya nahospitali atahakikisha analimaliza Kwa kuwatafutia wateja na kuwasemea nakuwatangaza katika kila sehemu ambayo atakuwa anaenda.
Kwa upande wake mkurugenzi wa tasisi hiyo Muhandisi Fredrick Kahimba alisema kuwa wamepokea maelekezo hayo na wapo tayari kuyafanyia kazi Kwa Kasi kama vile serikali ilivyoagiza
Kahimba alisema kuwa katika taasisi hiyo wamekuwa wakipata tatizo la kupata wateja wa vitanda wanavyovitengeneza Kwa ajili ya hospital kwani wametengeneza vitanda lakini tatizo kubwa walilonalo ni sehemu za kuviuzia ambapo alifafanua kuwa vitanda hivyo pamoja na vifaa tiba vingine walivyotengeneza vimeshapimwa na Kupata idhibati kutoka taasisi husika ikiwemo TMDA.
Aidha pia alisema kuwa kutengeneza vifaa tiba hivyo vimesaidia kuongeza ajira za ndani na kurahisha upatikanaji wa bidhaa kirahisi na kwa bei nafuu huku akifafanua kuwa kwa sasa TEMDO inavifaa tiba zaidi ya kumi na tano (15) ambapo pia alizisihi taasisi za serikali na binafsi kujitokeza Kwa wingi kwenda kuagiza vifaa tiba hivyo.