Ticker

6/recent/ticker-posts

MASHAMBA YATAKAYO BAINIKA NA MADAWA YA KULEVYWA AINA YA BANGI YATATAIFISHWA KWA AJILI YA MATUMIZI YA UMMA


 


Kamishna jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya ,Gerald Kusaya amesema mashamba yatakayobainika na madawa ya kulevya aina ya bangi yatataifishwa kwa matumizi ya umma ili kukomesha biashara hiyo.






Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Kamishna Kusaya alisema kutoakana na vitendo vya uzalishaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi kuendelea wataanza kutaifisha mashamba hayo ili kukomesha biashara hiyo.








Kamishna alisema wamekuwa wakiwakamata mara kwa mara baadhi ya watu lakini bado wanaendelea kuzalisha bangi kwenye mashamba hivyo sasa hivi serikali imeanza mkakati huo wa kuyataifisha.








Aidha amesema kuwa mashamba hayo yatakuwa yanakabidhiwa katika serikali ya vijiji ili maeneo hayo yaweze kutumiwa kwa matumizi ya umma na wananchi watajipangia kwa matumizi yao sahihi ya maeneo hayo.








"Kuanzia mei 20 hadi 23,2022 mamlaka hii kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani Arusha ilifanikiwa kuteketeza hekari zaidi ya 21 ya mashamba ya dawa za kulevya aina ya bangi,"alisema.






Vilevile alisema katika oparesheni hiyo takribani kilo 220 za bangi zilikamatwa katika eneo la usariver wilaya ya Arumeru na wilayani Monduli mkoani humo ikiwa hadi sasa watu wanne wanashikiliwa kwa tuhuma za kuzalisha na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.






Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za watu wanajihusisha na uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya ili kufikia Tanzania yenye kizazi kisichotumia wala kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya

Post a Comment

0 Comments