Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI ZA KIRAIA WAOMBA SERIKALI KUPITIA UPYA SHERIA YA MAKOSA YA UHALIFU WA BIASHARA YA BINADAMU

 


Mkurugenzi wa TRI,Edwin Mugambila akiongea na waandishi wa habari 


Wadau kutoka asasi za za kiraia wameiomba serikali kupitia upya Sheria ya makosa ya uhalifu wa biashara ya binadamu ili kukomesha vitendo hivyo kwani iliyopo inatoa mwanya kwa watuhumiwa kuendelea na biashara hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya inayohusika na haki za binadamu(TRI) Edwin Mugambila katika mafunzo  ya siku nne kwa maafisa wa serikali wanaosimamia sheria katika kuwajengea uwezo kwenye kupambana na kuzuia usafirishaji Haram wa binadam yaliyofadhiliwa na mfuko wa kimarekani la Hans Seidel.

Mugambila alisema kuwa Sheria hiyo ya makosa ya uhalifu wa kibinadamu inatoa mwanya wa kuendelea kutokana na adhabu ndogo wanayopewa watuhumiwa hasa ya kulipa faini au kifungo kidogo kisichozidi miaka 20.

"Mtu anaejihusisha na biashara hii ya tatu kwa kuingiza fedha nyingi ambayo kwa mwaka uliopita ripoti ilionyesha wahusika wanaingiza zaidi ya bilioni 150 kwa mwaka"alisema Mugambila 

 Lungambila alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuondoa faini na kuongeza kifungo kisichopungua miaka 30 ili kukomesha biashara hiyo haramu tofauti na sasa Watuhumiwa wanahukumiwa chini ya kifungo Cha miaka 20 au kulipa faini ya shilingi milioni mbili


Kwa upande wake, aliyekuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo, katibu wa sekretarieti ya kuzuia na kupambana na uhalifu wa usafirishaji wa binadamu Seperatus Fella alisema kuwa biashara hiyo inatishia maendeleo, amani, ukuaji wa uchumi na Hali ya kiusalama duniani hivyo kuwataka maafisa hao kuzingatia mafunzo kukomesha biashara hii.

"Kwa mujibu wa taaarifa ya serikali ya Marekani, inayotelewa kila mwaka juu ya biashara ya binadamu duniani, tafiti na ripoti za kimataifa Tanzania ni chanzo , mkondo na nchi kusudio la safari ya wanaume, watoto na wanawake kwa Ajira za kulazimishwa na biashara za ngono kwa kigezo Cha Ajira na elimu" 

Fella alisema kuwa Sheria mbali mbali zimetungwa nchini kukomesha biashara hii, lakini uelewa mdogo wa waendesha mashitaka  wa kuandaa hati za makosa haya ndio imekuwa changamoto kubwa katika vyombo vyetu vya kisheria kutoa haki na adhabu stahiki kwa washitakiwa.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Aisha Ndosi, hakimu wa mahakama kuu Kanda ya Arusha alisema kuwa wao wanafuata miongozovya Sheria na taratibu katika kuamua hatma ya kesi hizo.

"Sisi kama wasimamizi wa Sheria tunashindwa kupokea matokeo chanya kutokana na ufinyu wa upelelezi yanayofanyika na wanasheria wa serikali ambao ni wasaidizi katika kuendesha kesi hizo hivyo ikiwana changamoto tunashindwa kutenda haki Kama jamii inavyotutegemea"

Post a Comment

0 Comments