WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA UVIKO 10 KWA VYAMA VYA UTALII

 Katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii Dkt Francis Michael amegawa vifaa vya kujikinga na Uviko 19 ikiwemo barakoa 140,000 na vitakasa mikono 14,285 kwa vyama vya utalii ikiwa ni maandalizi ya kupokea idadi kubwa ya watalii hapa Nchini


 Alifanya zoezi hilo la ugawaji wa vifaa hivyo leo jijini Arusha wakati alipokutana na wadau wa utalii 

Alisema kuwa jitihada mahsusi za Mh Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania za kutangaza Tanzania kimataifa kupitia programu maalumu ya Royal tour ambayo imeenda sambamba na kuimarisha mapambano dhidiya ya UVIKO 19

Dkt Francis alisema kuwa wizara imejipanga kushirikiana na wadau ili kuendeleza programu ya Royal tour kwa lengo la kuvutia watalii kutoka masoko mbalimbali kutembea Tanzania na kuongeza mapato

Pia alisema kuwa kutokana na ushawishi wa Mh.Rais serikali ilipokea fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko ambapo sehemu ya fedha hizo zimetumika kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini 

"Fedha hizo zimetumika kukarabati kilometa 2,383.12 za barabara katika maeneo ya hifadhi za Taifa ikiwemo mapori ya Akiba,Tengefu na misitu ya hifadhi ya mazingira ya Asili"Aliaema Dkt Francis 

Aliongeza kuwa fedha hizo za uviko zimekarabati viwanja vya ndege katika hifadhi za Taifa pamoja na kujenga malango 14 ya kupokelea wageni katika maeneo ya hifadhi sambamba na kuboresha mazingira ya biashara 

Kwa upande wake katibu mtendaji wa shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania Richard Rugimbana akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya vyama hivyo alisema kuwa ni vyema msaada huo ukatumika kwa malengo yaliyokusudiwa

"Hapa mbele yako Mh Katibu Mkuu tuna vyama 10 na hivi vyama vidogo ndivyo vinakutana na watalii na mfano mzuri ni namna wanavyowapandisha watalii mlima Kilimanjaro na maeneo mengine ya utalii"alisema Rugimbana

Alipongeza Serikali katika jitihada za kutangaza utalii sambamba na kuchukua tahadhari za Uviko 19

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post