Rais wa TLS Dr. Edward Hosea akimkabidhi waziri wa katiba na sheria Damas Ndumbalo Muhuri wa kilieletroniki Kwa ajili ya kuuzindua rasmi Leo katika ukumbi wa Simba uliopo katika kituo Cha mikutano Cha AICC mkoani Arusha ambapo waziri huyo alitoa akizo kwamba Baada ya siku 30 wanasheria wote wawe wanatumia mihuri hii yakieletroniki
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Ili kuhakikisha tatizo la wanaotumia mihuri ya mawakili kiholela (vishoka ) wanamalizika chama cha mawakili Tanzania (TLS)kimekuja na mihuri mipya ya kieletroniki ambayo itatolewa Kwa wanachama hai na ambayo itazibitiwa na chama hicho.
Akitoa Maelezo ya mihuri hiyo katika mkutano mkuu wa chama Cha mawakili Tanzania (TLS) Capt.Ibrahim Bendera alisema kuwa mihuri hii mipya itasaidia kuwathibiti vishoka wote ambao walikuwa wanatumia mihuri ya kawaida kiholela pamoja na wale ambao walikuwa wanavunja sheria na maadili ya taaluma ya uwakili.
Alisema kuwa ili Kuthibiti uharibifu ambao sio sahii wameona watumie mihuri hii ya kieletroniki ili kuwathibiti vishoka hawa ambapo alisema mihuri hii ukigonga unaweza ukaonyesha taarifa zote za mgongaji ikiwemo ya kuwa ni wakili wawapi je ni wakili ambaye amesajiliwa na chama na je anafanyia kazi zake wapi.
Alibainisha kuwa wao kama mawakili wamekubaliana na uwamuzi wa wizara waliotoa wa kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja Kila wakili ana tumia Muhuri huo.
Akifungua mkutano huo Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro Ndumbalo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita ikiongoswa na mama Samia Suluhu Moja ya ajenda zake ni kushirikiana na sekta binafsi ,sekta za umma pamoja na tasisi mbalimbali
Alibainisha kuwa Kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko ya watu kujifanya mawakili na kutumia mihuri ya mawakili kutokana na hilo amefurahi kuona TLS imepata ufumbuzi wa swala hilo Kwa kuleta mihuri ya kieletroniki ambayo anaamini itaenda kumaliza tatizo hilo
Alisema kuwa wao kama watunga sera ,kama wizara ya katiba na sheria ambayo TLS ipo chini yake wanatoa maelekezo kwamba ndani ya siku 30 mawakili wote wawe na mihuri ya kieletroniki baada ya hapo hawatatambua mihuri yote ambayo sio ya kieletroniki
Alibainisha kuwa baada ya siku izo 30 wataandikia Mamlaka zote ambazo zinatambua mihuri ya mawakili ikiwemo TRA na wadau wengine baada ya siku 30 kuanzia leo wasitambue Muhuri wowote wa mawakili isiokuwa wa kieletroniki
Alisema kuwa anatambua kuwa TLS kuwa ni chombo kinachoshauri serikali hivyo katika utoaji ushauri wao waangalie namna au njia sahihi ya kushauri serikali njia ambayo itaifanya serikali kijisikia vyema na sio kuifedhehesha serikali.
Kwa upande wake Rais wa chama Cha mawakili Tanzania Dr Edward Hosea amesema kuwa mkutano huo umekutanisha mawakili wote kutoka Tanzania ambao ni wanachama.
Amesema kutakuwa na mada tofauti zitakasowakilishwa na mawakili na kwamba wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kushirikiana na serikali ili waweze kutimiza majukumu yao kama nchi.
Amesema wamekuwa wakifanya mkutano huo kila mwaka na wanatarajia kujadili mada ambazo zitaleta tija na ufanisi katika chama hicho.
Rais wa TLS Dr. Edward Hosea akimkabidhi waziri wa katiba na sheria Damas Ndumbalo Muhuri wa kilieletroniki Kwa ajili ya kuuzindua rasmi Leo katika ukumbi wa Simba uliopo katika kituo Cha mikutano Cha AICC mkoani Arusha ambapo waziri huyo alitoa akizo kwamba Baada ya siku 30 wanasheria wote wawe wanatumia mihuri hii yakieletroniki
Katika mkutano huu wa mawakili waziri wa katiba na sheria ameweza kuzindua njia ya mtandao ya kupiga kura za kumchagua Rais wa TLS ,pamoja na kuzindua rasmi saccos ya chama hicho itakaowashirikisha mwanachama yeyote wa TLS.