Ticker

6/recent/ticker-posts

HIZI HAPA AJIRA ZAIDI YA LAKI MBILI ZILIZOTANGAZWA NA SERIKALI KWA AJILI YA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA

 Na Janeth Bocco - Dodoma

SERIKALI imesema mchakato wa kuwapata makarani na wasimamizi wa Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ,umeanza leo Mei 5 hadi Mei 19 mwaka huu ambapo waombaji ni wenye umri Kati ya miaka 18 hadi 45 ambapo mahitaji ni makarani laki mbili na elfu tano[205,000] wanahitajika

Aidha Serikali imewaonya watu wenye nia isiyo njema kwa zoezi la sensa ambao wamekuwa wakijaribu kutoa matangazo ya ajira za Sensa kwa nia ya kluwatapeli wananchi wanaohitaji kushiriki katika zoezi la Sensa huku ikielezwa kuwa kwa wote watakaobainika watasakwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge Sera,uratibu ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu George Simbawene ameyasema hayo leo Mei 5,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajira hizo za muda katika maandalizi ya kuelekea kwenye Sensa.

Amesema,ajira  hizo zitaombwa kupitia mtandao na hazitahusisha malipo ya aina yoyote kwa mwombaji wa ajira  huku akisema mchakato wa kuchambua maombi ya kazi pamoja na usaili utasimamiwa na Kamati Maalum itakayoundwa katika ngazi ya kila wilaya.

Aidha amesema usaili utafanyika katika ngazi ya wilaya kwa wasimamizi wa TEHAMA .

“Niwaombe watanzania wote wenye sifa ambao wangependa kuomba nafasi za ajira za makarani na wasimamizi wa sensa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ukamilifu ili kuomba nafasi hizo ambazo kazi za kufanya pamoja na sifa za mwombaji zimebainishwa katika tangazo la ajira za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022.”amesema Simbachawene na kuongeza kuwa

“Mfumo wa kuomba ajira hizi kupitia mtandao unapatikana kupitia www.pmo.go.tz,www.tamisemi.go.tz,www.nbs.go.tz kwa Tanzania Bara na www.ompr.go.tz,https//www.tamisemim.go.tz au www.ocgs,go.tz kwa wale wanaoomba Tanzania Zanzibar na kupitia tovuti hizo waombaji watapata tangazo kamili la kazi lenye orodha ya nafasi zilizopo katika sense pamoja na vigezo vinavyohitajika.”

Naye Kamisaa wa Sensa Anne Makinda ambaye pia ni Spika Mstaafu ametoa wito kwa wenyeji wa maeneo husika kuomba nafasi hizo za ukarani ili kurahisisha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge Sera,uratibu ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu George Simbawene akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ajira za muda  za makarani wa sensa.
Kamisaa wa sensa Anne Makinda akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi

Post a Comment

0 Comments