Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAWAKARIBISHA WANAHISA WA BENKI HIYO ,GAWIO LAKUKATA NA SHOKA LAPENDEKEZWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha ripoti ya mwaka 2021 ya Benki ya CRDB, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha wenye lengo la kuwakaribisha wanahisa wa benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Wanahisa unaotarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 21/05/2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), na kupitia mtandao.  Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha, kuwakaribisha wanahisa wa benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Wanahisa unaotarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 21/05/2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), na kupitia mtandao. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.

=======   =======   =======

Benki ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 27 wa Wanahisa siku ya Jumamosi tarehe Mei 22 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Mkutano huo unafanyika kufuatana na Sheria ya Makampuni namba 212 ya mwaka 2002, ambapo kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu huo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, na kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2022 ambapo pendekezo la gawio kwa mwaka huu ni Shilingi 36 kwa hisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 64 kulinganisha na Shilingi 22 kwa hisa iliyotolewa mwaka uliopita.

Pendekeo hilo la ongezeko la gawio kwa hisa linatokana na Benki ya CRDB kuendelea kupata matokeo mazuri sokoni ambapo mwaka wa fedha ulioisha ilipata faida kabla ya kodi ya Shilingi Bilioni 387 ukilinganisha na Shilingi Bilioni 236 mwaka 2020.

Akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema mkutano huo pia utafanyika kidjitali “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki kwani sio wote wanaweza kufika Arusha siku hiyo.

“Kwa kuzingatia uzoefu tulioupata kwa kufanya mkutano wa 26 ambao ulifanyika kwa mara ya kwanza kwa kwa njia zote mbili. Mwaka jana Wanahaisa walipitisha kuendelea kutumia njia zote mbili za kuendesha mkutano kwa mwaka huu 2022,” alisema Nsekela

Aliongezea kuwa pamoja na kuwa utaratibu huu ni matokeo ya changamoto ya janga la corona, lakini umekuwa na manufaa katika kuwawezesha Wanahisa wengi kupata haki yao ya msingi ya kushiriki mkutano.

Mtandaoni Wanahisa wataweza kujiunga kuanzia saa 2:00 asubuhi kupitia link https://escrowagm.com/crdb/login.aspx au kupitia SimBanking App, ambapo imewekwa sehemu ya ya kujisajili kushiriki Mkutano Mkuu. 

“Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” alisema Nsekela huku akiwahkikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.

Mkutano Mkuu wa 27 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa yake ili kukuza uelewa wa masuala mbalimbali ya fedha na uwekezaji katika masoko ya mitaji. Semina hiyo itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 21/05/2022 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Mgeni Rasmi katika semina hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Mwigulu Nchemba ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wa masuala ya fedha, sheria na uwekezaji katika masoko ya mitaji. “Nachukua fursa hii kuwakaribisha wanahisa wote katika semina na Mkutano mkuu niwasihi wajitokeze kwa wingi kwani hii ni haki yao ya kimsingi na kisheria,” aliongezea.

Akielezea kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ya “Thamani Endelevu”, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Mwambapa alisema inaelezea ni kwa namna ambavyo Benki yetu imekuwa ikiimarika katika utendaji, na hivyo kupelekea ukuaji. 

“Kama ambavyo ameeleza Mkurugenzi Mtendaji mwaka huu Bodi imekuja na pendezeko la gawio la Shilingi 36 kwa hisa sawa na ongezeko la asilimia 64, hii ni kiashiria tosha kuwa kumekuwa na thamani endelevu katika uwekezaji wa Wanahisa wetu,” alisisitiza Tully.

Toa Maoni Yako:

0 COMMENTS SO FAR,ADD YOURS

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Post a Comment

0 Comments