Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKULIMA WADOGO NA BINAFSI WA MIWA WAONDOKANA NA CHANGAMOTO YA KUTENGENEZA SUKARI




Na Woinde Shizza , ARUSHA 
Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) imekuja na suluhisho Kwa ajili ya wakulima wadogo na binafsi wa miwa nchini ambao wanakabiliwa na tatizo la kukosa masoko ya bidhaa zao baada ya taasisi hiyo kutengeneza mitambo midogo yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 Kwa siku za sukari .


Aidha pia mitambo hiyo ambayo imebuniwa kwa ajili utengenezaji sukari kwaajili ya wajasiriamali mdogo inauwezo wa kutengeneza tani 20 kwa siku moja pia inauwezo wa kuchangia wastani wa tani 3000 hadi tani 3600 Kwa mwaka katika soko la sukari.




Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa tasisi hiyo Muhandisi Fredrick Kahimba alisema kuwa wameamua kuja na mashine hiyo Ili kuweza kumrahisishia mjasiriamali mdogo kazi na kumpunguzia gharama.

Alibainisha kuwa mara nyingi viwanda huwa vinavuna kwanza miwa yao kisha uangalia iwapo wanahitaji miwa zaidi kutoka kwa wakulima binafsi ambayo mara nyingi ni sehemu ndogo tu hivyo wakulima wengi wamekua wakikosa soko.


 Alisema kuwa utengenezaji wa mashine hizo umekuwa mkombozi kwa wakulima wa miwa nchini ambao wataondokana na utegemezi wa kuuza miwa yao viwandani na kuanza kuchakata miwa yao kwaajili ya kuzalisha sukari ambayo kwa nyakati tofauti nchi imekua ikipata upungufu.

"Utengenezaji wa mashine hizi utasaidia Kwa kiasi kikubwa sana Kwa kupunguza upatikanaji wa sukari haswa katika tatizo la upatikanaji"alibainisha



Aidha pia alisema mbali na hilo pia wameamua kubuni mashine ya kusafisha na kuchuja mafuta ya alzeti yenye uwezo wa kusafisha mafuta lita elfu moja Kwa siku ambapo pia itamsadia mkulima kuweza kuvuna alizeti yake kuikamua na kuisafisha Kwa ajili ya kuiuza pamoja na kutumia 

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TEMDO Dkt.Richard Masika alisema kuwa mashine zote hizi zinapatikana katika taasisi hiyo na upatikanaji wake unaendana na gharama ambazo mtanzania yeyote anaweza kuzimudu.

Post a Comment

0 Comments