Polisi akiingia bora
Baadhi ya Polisi wa doria ya Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora.
*****
Watu
wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamepora begi linalodaiwa kuwa na
fedha kisha kumpiga risasi ya shingo mwendesha boda boda na kupora
pikipiki yake nje ya Kiwabnda cha Bora, baranara ya Njerere Dar es
Salaam mchana huu.
Father
Kidevu Blog ilifika eneo la tukio na kukuta watu wakielezea tukio hilo
na kulifabnanisha na la sinema kutokana na kile walichokiona.
"Tuliona
mzee mmoja tunahisi ni mfakazi wa Bora, alifika na pikipiki hapa,
wakati anataka kuingia ndani wakafika watu wengine wawili katika
pikipiki na kuamuru kupewa begi lile na ghafla mwenda pikipiki akawa
anawahoji inakuaje wanachukua begi hilo ndipo tukasikia mlio wa risasi
na bodaboda yule akaanguka chini wakamsukuma na kuchukua pikipiki yake
na kukimbia nayo," alisema shuhuda yule.
Polisi
ilifika eneo la tukio huku wengine wakiendelea na msako mkali dhidi ya
wahalifu hao wakutumia sihala huku hofu ya kijana yule wa boda boda
kupoteza maisha ikiwa kubwa kutokana na eneo alilopigwa risasi.